Mkuu wa Wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah wa kwanza kushoto akikapata utepe kuashiria makabidhiano ya mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde,Shule ya Msingi Mdote na Soko la Majengo wilayani Muheza uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Kulia Diwani wa Kata na anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani.
Na Oscar Assenga, MUHEZA
MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa ) wamesema katika
kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Serikali imewawezesha
ujenzi wa miradi ya kimkakati 20 ya maji safi yenye thamani ya zaidi ya
Bilioni 161 ambayo imekuwa chachu kubwa kuwezesha wananchi kupata
huduma ya maji safi na hivyo kuondokana na changamoto walizokuwa nazo
awali.
Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban wakati
wamekabidhi mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani Muheza
pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi wa
Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde,Shule ya Msingi Mdote na Soko la
Majengo wilayani Muheza.
Mhandidi Shaban alisema pamoja na hilo
pia ipo miradi 6 ya maji taka yenye thamani ya Bilioni 4.2 ukiwemo wa
ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kuchakata majitaka wenye thamani ya
Bilioni 1 ambao umetekelezwa na hivyo kusaidia kuondosha kero ambayo
ilikuwa ikiwkumba wananchi.
Alisema kutokana na uwezeshwaji huo
kwa sasa mamlaka hiyo inatoa huduma ya maji safi na salama kwa wastani
wa asilimia 92.5 ya wakazi wa Jiji la Tang (96.1%), Pangani (70%) na
Muheza (71%) ambapo miaka mitatu iliyopita kabla ya utawala wa Serikali
ya awamu ya sita huduma ya maji ilikuwa inapatikana kwa wastani wa
asilimia 83.2 ya wakazi hao (Tanga 89%, Muheza 33% na Pangani 60%).
Aidha
alisema hivi sasa maji safi yanapatikana kwa wastani wa saa 15 kwa siku
katika miji ya Muheza ambapo miaka mitatu iliyopita huduma ya maji
ilikuwa inapatikana kwa wastani wa masaa matatu na wakati mwengine siku
moja baada ya Juma Zima.
Akizungumzia huduma ya uondoshaji wa
maji Taka, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema huduma hiyo hufanywa kupitia
mtandao wa mabomba unaowahudumia wakazi wapatao 20,615 sawa na asilimia
5.2 ya wakazi Tanga Mjini, Maeneo ya Muheza, Pangani na maeneo ya
pembezoni mwa Jiji la Tanga ambayo hufanywa kwa kutumia mifumo mingine
ya uondoshaji majitaka ikiwemo vyoo vya shimo na vyoo vya kunyonywa na
magari vikishajaa.
Hata hivyo akielezea ujenzi wa vyoo na ombi la
kukabidhi kwa watumiaji ,Mhandisi Rashid alisema kwamba kwa kua mradi
huo unahusiana na usafi wa mazingira,Tanga Uwasa iliona ijenge aina hiyo
ya vyoo ili kuonesha mfano wa vyoo bora vinavyotakiwa kujengwa katika
jamii ikiwemo faida ambazo zinapatikana kupitia mradi huo.
Alisema
faida ni kuwaepusha uchafuzi wa maji ya ardhini, uwepo wa huduma karibu
na wananchi kupitia gari la kunyonya majitaka toka na hivyo kuondoa
changamoto ya utupaji mbali na wakati mwengine katika maeneo
yasiyorasmi.
“Pia kupungumza changamoto ya ufinyu wa vyoo katika
shule za Msingi Mdot,Shule ya Sekondari Bonde na Soko la Majengo ambapo
gharamaa nafuu kwani kutumia eneo dogo la ardhi na hudumu muda mrefu pia
upatikanaji wa mbolea inayoweza kutumika kwa kilimo lakini tunaishukuru
Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kuwezesha ujenzi wa mradi
huu”Alisema
“Sisi Tanga Uwasa tumeona ujenzi wa vyoo umekamilika
na vipo tayari kutumika tunadhani hakuna haja ya kuendelea kusubiri hadi
ujenzi wa miundombinu pale Kilapula ukamilike ikiwa wanafunzi na
wananchi sokoni wanauhitaji mkubwa hivyo tunakuomba ukabidhi vyoo hivi
kwa uongozi wa shule ya Sekondari Bonde, Shule ya Msingi Mdote na Soko
la Majengo vianze kutumika na hivyo kusaidi kupunguza changamoto iliyopo
ya uhitaji wa matundu ya vyoo”Alisema
Awali akizungumza mara
baada ya kupokea mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji Taka wilayani
Muheza pamoja na kukabidhi Vyoo vilivyojengwa ikiwa ni sehemu ya Ujenzi
wa Mradi huo kwa shule ya Sekondari Bonde, Shule ya Msingi Mdote na Soko
la Majengo wilayani Muheza, Mkuu wa wilaya ya Muheza ZainabuAbdallah
alisema miaka mitatu ya nyuma hali ya upatikanaji wa maji ilikuwa ni
asilimia 33 lakini miaka mitatu sasa hivi himefikia 71 hiyo ni kazi
kubwa anayoifanya Rais Dkt Samia Suluhu.
Katika miaka mitatu ya
Rais Dkt Samia wamefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya kikamkati 20
yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 161.4 ya Maji Safi na Maji Taka miradi
sita yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 4.2 ambapo hiyo ni kazi kubwa na
nzuri inayofanya na Rais Samia.
Alisema wamefika katika hafla
hiyo kuungana na Tanga Uwasa katika tukio hilo huku akimpongeza Waziri
wa Maji Jumaa Aweso kutokana na kazi kubwa anayofanya kuhakikisha huduma
ya maji kwenye mkoa wa Tanga inakuwa nzuri na Muheza wanatekeleza mradi
mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya maji taka wenye thamani ya zaidi ya
Bilioni 1 ambapo kwenye mradi ho wamepata gari la maji taka, gari ya
usimamizi wa mradi na wamepata matundu ya vyoo,shule ya sekondari na
Msingi pamoja na Soko .
No comments:
Post a Comment