March 29, 2024

Dkt. Muchunguzi : Miaka Mitatu ya Rais Samia Demokrasia imeimarika

 Na Hellen Ngoromera

 

MCHAMBUZI wa masuala ya kisiasa nchini, Dk. Denis Muchunguzi amesema miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan  imeimarisha na kukuza demokrasia nchini.

Dk. Muchunguzi amesema hayo jana Machi  26 wakati akiwasilisha mada katika mjadala wa uchambuzi wa miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia madarakani ulioandaliwa na Kampuni ya Mchambuzi Media..

"Napongeza miaka mitatu ya  Dk. Samia kwani amefanya makubwa... tumeshuhudia mikutano ya kisiasa ikiruhusiwa, maandamano ya Chadema kwenda Umoja wa Ulaya yalifanyika bila bugudha," amesema Dk. Muchunguzi.

Amesema pia  hata baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa waliohama nchini kutoka  na  sababu mbalimbali walirejea nchini.

Jambo lingine ni pamoja na  kuruhusiwa kwa mitandao ya kijamii ambayo ilipigwa marufuku.

 Ameshauri vyama vya siasa kuwa imara na madhubuti kifedha ili viweze kujiendesha vyema.

"Vyama vya siasa viwe imara kifedha, hatuhitaji kuona vyama vinakufa," amesema Dk Muchunguzi.

 Akichangia mada ya Uchumi na Miradi ya Maendeleo,  Profesa Samuel Wangwe,  ameshauri serikali kuboresha maisha ya wananchi ili kuwakwamua kiuchumi.

Profesa Wangwe amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia mdarakani ameweze kuinua uchumi na kufikia asilimia 5.2 na kwamba ana imani  kiwango cha ukuaji wake kitaingezeka kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages