March 18, 2024

ESWLT watoa msaada wa wa vifaa tiba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

Umoja wa Wanawake Viongozi na Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali (ESWLT) umetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma  ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.



Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Hospitalini hapo na kutembelea katika wodi ya wakinamama Katibu wa Umoja huo Sakina Mwinyimkuu amesema kuwa kitendo cha kutoa vifaa hivyo ni miongoni mwa malengo yao ya kusaidia jamii.

Katibu wa umoja huo Mwinyimkuu amesema wamekabidhi Jumla ya mashuka 400 na kuongeza Tumechangia kwa umoja wetu kila mwanachama amechangia alichonacho kwa nguvu yake kwa uwezo wake,tumeweza kupata mashuka 400 ambayo tumeyagawa leo hapa"Amesema Mwinyimkuu

Aidha amesema kuwa Umoja huo una lengo la kusaidia vijana Wanawake hasa mabinti ambao wanatarajia baada ya miaka kadhaa wataingia katika Utumishi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kusaidia jamii.

"Malengo manne ya umoja huo ni kuwajengea uwezo viongozi wanawake kutoka katika taasisi mbalimbali kusaidia viongozi vijana ili kuwaandaa katika uongozi na kutoa fursa Kwa wastaafu kusaidia jamii"amesema

Pia wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushikiria ajenda ya mama na wao ni Wanawake hawana namna yoyote zaidi ya kuungana nae kwa nguvu zote ili waweze kufanikisha ajenda hiyo.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe ameushukuru umoja wa Wanawake hao kwa kuchagua eneo hilo kutoa msaada huo kwa sababu eneo walilolichagua ni eneo nyeti

"Kina mama wanaojifungua pamoja na watoto wao wanahitaji Sana mashuka  safi ili kuzuia maambukizi ya magonjwa"Amesema

Kwa upande wake Rashida Mfaume mjumbe katika Umoja huo wa Wanawake Viongozi amesema kuwa katika kutoa msaada mwaka huu wameangazia katika sekta ya Afya hususani katika eneo la mama na mtoto na mashuka yametolewa masafi kwa ajili ya wodi za wazazi.

Kwa Upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya kina Mama kutoka hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dk Enerd Chiwanga amesema walikuwa na mahitaji makubwa ya mashuka hivyo wanashukuru umoja huo kwani watapunguza changamoto iliyopo.



No comments:

Post a Comment

Pages