HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 31, 2024

HATIMAYE YAMEKUWA, AHLY ASHIDA LUPASO

Na John Marwa


MNYAMA Simba ameshinda kutamba nyumbani mara baada ya kukubali kichapo cha bao 0-1 dhidi ya Miamba ya Soka la Afrika usiku wa leo.




Ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL ambapo kwa mara ya kwanza Mabingwa watetezi wanashinda Benjamin Mkapa katika historia ya michezo ya hivi karibuni.

Makosa ya walinzi wa Simba Ahly ealiyatumia vyema baada ya kutumia mpira uliokua ukizagaa langoni mwao licha ya jitihada za Ayoub Lankred lakini Ahly walikipatia bao la uongozi na la ushindi katika mchezo wa leo.

Yawezekana ikawa siku mbaya zaidi kwa nyota wa Simba kwenye mchezo wa kwa kushindwa kutumia nafasi zaidi ya tano walizozitengeneza.

Simba baada ya kuruhusu bao walichukua mchezo na kumiliki maeneo mengi ya Uwanja lakini walishindwa kuzitumia nafasi hizo.

Mchezo wa marejeano utapigwa juma moja lijalo Dimba la Cairo International jijini Cairo Misri.

Simba anahitaji kwenda kushinda mechi inayofuata Ili kuweza kutinga hatua ya Nusu Fainali.

 

No comments:

Post a Comment

Pages