KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment
Committee-PIC), imeridhishwa na uwekezaji wa jengo la kitega uchumi la PSSSF
Commercial Complex, lililoko barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam.
Jengo
hilo la kisasa lenye ghorofa 35 linamilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) na kwa sasa tayari limekamilika kwa asilimia 100 na
limeanza kutumika.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya PIC ya kutembeela mradi huo wenye thamani
ya shilingi bilioni 232, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge Mhe. Deus
Sangu amesema, Kamati imekagua mradi na kujiridhisha kuwa ni mzuri na
umetekelezwa kwa viwango vyote vinavyohitajika.
“Sisi
kama kamati tumeendelea kuishauri PSSSF kuhakikisha jengo hili ambalo limewekeza
fedha nyingi za Mfuko linasimamiwa na tija iliyokusudiwa inapatikana, tumekagua
na tumeridhika na uwekezaji huu na tunaiponegza PSSSF.” Amesema.
Amesema
Kamati yake imeelekeza katika kipindi cha matarajio ya chumo la uwekezaji (Return
of investment) inaleta tija na kupata chumo ndani ya muda iliyojiwekea kisha kuanza
kupata faida.
“Na
hii itakuwa ni faida kwa Mfuko na kuufanya uweze kuendelea kuwahudumia
wananchama bila kutetereka.” Alisema.
Mwenyekiti
huyo amempngeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, kwa namna anavyosukuma mabadiliko ya kiuchumi nchini na uwekezaji huo
umeakisi R mbili kati ya zile nne za Mhe. Rais ambazo ni Reforms na Rebuild.
Naye
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Pius Chaya, licha ya kupongeza uwekezaji huo
lakini pia ameishauri serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kuangalia
uwezekano wa taasisi za umma ambazo ziko Dar Es Salaam kutumia jengo hilo.
“Hatuui
taasisi binafasi lakini ipo haja ya kujaza nafasi zilizobaki.” Amefafanua Dkt.
Chaya.
Akitoa
wasifu wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru amesema jengo
la PSSSF Commercial Complex ni jengo refu zaidi na ni moja ya alama za jiji la
Dar Es Salaami, ni jengo refu sana katika nchi za Afriak Mashariki na Kusini
mwa Afrika.
Amesema
jengo hilo lina minara mmitatu (towers) moja ni Commercial Complex ambalo ni refu zaidi lenye ghorofa 35 Executive tower lenye ghorofa 14 na eneo
la maegesho lenye ghorofa 6.
“Hapa
ndio panaitwa PSSSF Commercial Complex, kuna Executive tower ambako ni maalum
kwa shughuli za maofisi, commercial complex linahusisha mabenki, ofisi
mchanganyiko na kumbi za mikutano na shughuli nyingine za kijamii, lakini pia
kuna ene la maegesho ya magari.” Amefafanua.
Amesema
jengo hilo limeendelea kuwavutia wapangaji wengi zaidi kadiri muda unavyokwenda
na matarajio ya Mfuko, kufikia desemba mwaka huu 2024, kiwango cha upangishaji
kinatarajiwa kupanda na kufikia asilimia 70.
Amesema,
miongoni mwa wapangaji mashuhuri kwenye jengo hilo ni pamoja na Shirika la
Umoja wa Mataifa (UNDP) na taasisi zake, kampuni kubwa ya mitandao ya simu Tigo,
taasisi za umma, mabenki na wafanyabiashara binafsi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment
Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu, akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua
mradi wa jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex, lililoko
barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam, Machi 21, 2024.
Mkurugenzi
Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa
jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma
jijini Dar Es Salaam, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), wakati wa ziara ya
wajumbe wa kamati ya PIC kukagua jengo, Machi 21, 2024.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima (Aliyesimama), akizungumza mbele
ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu
wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua
jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma
jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024.
Wajumbe
wa Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment
Committee-PIC), wakiongozwa NA Mwenyekiti wake Mhe. Deus Sangu na Menejimenti
ya PSSSF wakitembelea jengo la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma
jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024.
Taswira
ya jengo la kitega uchumi la PSSSF
Commercial Complex lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC),
wametembelea jengo hilo Machi 21, 2024, ili kukagua mradi huo uliogharimu Mfuko
wa PSSSF, kiasi cha shilingi Bilioni 232.
Majenereta ya usaidizi inapotokea umeme wa TANESCO umekatika
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment
Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (Katikati), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu
wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru huku Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF,
Bw. Rashid Mtima akishuhudia, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua
jengo la kitega uchumi la PSSSF
Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar Es Salaam Machi 21,
2024.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment
Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (Katikati), akipeana mikono na Mwenyekiti wa
Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima huku Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw.
Abdul-Razaq Badru, akishuhudia, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC),
kukagua jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam
Nujoma jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024.
No comments:
Post a Comment