Na John Marwa
KIMEUMANA, ndivyo unaweza kusema mara baada ya michezo ya mkondo wa kwana hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kutamatika huku hakuna aliyejihakikishia kufuzu.
Ni mara baada ya hapo jana kushuhudiwa michezo mitatu ambayo ilimalizika kwa suluhu, katika Dimba la Benjamin Mkapa wenyeji Yanga SC walitoshana nguvu na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Ulikuwa mchezo uliojaa mbinu nyingi kwa timu zote mbili lakini haikufua dafu kwa yeyeto kutikisa nyavu za mpinzani wake.
Yanga walipiga mashuti manne yaliyo lenga lango huku Mamelodi wakipiga mawili huku umiliki wa mchezo ukienda kwa Sundowns kwa asilimia 69, Yanga asilimia 31.
Mchezo wa marejeano ni juma lijalo nchini Afrika Kusini April 5 saa tatu kamili usiku.
Wakati Yanga wakitoa Suluhu na Sundowns mchezo wa mapema TP Mazembe walitoka suluhu dhidi ya Petro De Luanda ya Angola na mchezo wa mwisho wa Robo Fainali ulipigaa nchini Tunisia ambapo Esperance De Tunis walitoka suluhu dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Ukitazama Robo Fainali zote nne ni Simba tu walipoteza mchezo dhidi ya Al Ahly kwa bao moja kwa bila Uwanja wa Benjamin Mkapa hapo juzi.
Je ni nani kutinga hatua ya Nusu Fainali CAF CL ikiwa kila timu ina asilimia za kusonga mbele kama itazitumia dakika 90 za mkondo wa pili vyema?? KIMEUMANA bado ngoja tusubiri kuona ni Ahly ama Simba, ni Mamelodi ama Yanga, ni Petro ama TP Mazembe ama ni Asec Mimosas ama Esperance De Tunis?
No comments:
Post a Comment