March 26, 2024

MBUNGE KOKA AWAPONGEZA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM KWA MSHIKAMANO WAO

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa dhati wanachama wa ccm pamoja na wananchi wa Kata ya Pangani kwa kuweza kumchagua Yohana Gunze kuwa  diwani wa Kata ya Msangani katika uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni.

Koka ameyasema hayo wakati wa kikao màalunu  cha Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji chenye lengo la kujadili agenda mbali mbali kimaendeleo  pamoja na kujiandaa na chaguzi mbali mbali ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Alisema Koka aliwapongeza viongozi mbali mbali kuanzia ngazi zote za chini hadi ngazi za juu kwa ushirikiano wao wa  dhati katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi wa udiwani hadi uchaguzi mwenyewe. 

Koka alisema kwamba amefarijika sana kuona wanachama na wananchi kukiamini chama cha mapinduzi na kumchagua kwa kishindo  mgombea udiwani wa kata ya Msangani kwa kushinda kwa kishindo kwa asilimia 99.20

"Nawashukuru sana wanachama wenzangu wa ccm pamoja na wananchi wote kwa ujumla wa kata ya  Msangani kwa kuweza kukiamini chama cha mapinduzi na kuibuka na ushindi mkubwa katika kata ya Msangani hii inaonyesha ni jinsi gani tulivyokuwa na mshikamano,"alisema Mbunge Koka.

"Ni kweli nilikuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi lakini nashukuru kwa dhati viongozi na wananchi wa Jimbo la Kibaha kwa dua zenu na nashukuru Mungu nimerudi na nipo nanyi ili kuendeleza gurudumu la maendeleo,"aliongezea Koka.


Kadhalika Koka alibainisha kwamba wana CCM wote kwa sasa wanatakiwa kuwa na umoja na ushirikiano na kujipanga katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu  ili kuweza kushinda.

Pia alisema pamoja na kuwa nje ya nchi lakini amekuwa akiendelea kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo kushirikiana bega kwa bega katika kushauliana mambo ya maendeleo na kijamii,"alisisitiza Koka.

Katika hatua nyingine Koka alitoa pongezi kwa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika Jimbo la Kibaha mjini.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamaka amesisitiza umoja na mshikamano kwa lengo la kuweza kukiimarisha chama.

Kikao maalumu  cha halmashauri kuu ya (CCM) Wilaya ya Kibaha mji imeweza kukutana na kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kujiandaa na chaguzi mbali mbali za serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu.

               MWISHO

No comments:

Post a Comment

Pages