March 08, 2024

SAMIA, MWINYI USO KWA USO NA ACT-WAZALENDO KUHUSU UMOJA WA KITAIFA


Na Makuburi Ally

 


CHAMA cha ACT Wazalendo kinatarajia kuwakutanisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa lengo la kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (GNU).


Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu  alisema hatua hiyo imetokea kwenye kikao cha Halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho iliyokutana Machi 4 mwaka huu makao makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.


Alisema uwepo wa GNU ni utulivu wa kiuchumi, Utalii, mikopo, biashara kwani ni roho ya uchumi inayotegemea utulivu.


"GNU ni zao la damu ya Wazanzibar, kila uchaguzi watu hufa kwa wingi, mfano uchaguzi wa 2020, walifariki watu wengi kwa sababu ya vurugu za uchaguzi," alisema na kuongeza
Mnapozungumzia tamu ya GNU ni damu ya watu, kama halitazamwi jambo hili kwa jicho la pili, ndio maana tunataka kukutana mapema iwezekanavyo na Marais wote wawili.


Shaibu alisema katika Halmashauri Kuu Taifa ilifanya tafakuri ya kina juu ya mwenendo na mwelekeo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.


Alisema Serikali hiyo ni matakwa kisheria kati ya aliyekuwa kiongozi wa chama hicho, marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwa hoja tatu.


Alizitaja hoja hizo ni pamoja na kuachiwa huru kwa viongozi wote wa ACT walioshikiliwa kwa hila, watuhumiwa hao ni lazima wafidiwe sambamba na mageuzi ya kimfumo na usimamizi wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Pages