Na Hellen Ngoromera
MKOA wa Tabora umetajwa kuwa wa mwisho kwa idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika.
Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Ameir, ameeleza hayo jana Machi 13 wakati wa mafunzo ya Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es Salaam kuhusu usambazaji wa matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yaliyofanyika Dar es Salaam.
Amesema mkoa huo uko nyuma kwa watu hao kwa kuwa na asilimia 68.0 ya watu hao wasijua kusoma wala kuandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Kwa mujibu wa Ameir, Dar es Saam umekuwa kinara kwa kuwa na asilimia 97.5 ya watu hao.
Ameeleza kuwa matokeo ya Sensa matokeo ya Sensa ndiyo yanayowezesha mipango mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kufanyika.
Naye Mratibu wa Sensa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Kapala amesema tasnia ya habari ni muhimu ni muhimu kwa jamii kwani ndio nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi hivyo wanahabari wana wajibu wa kuhabarisha umma kuhusu msuala ya takwimu.
No comments:
Post a Comment