March 14, 2024

TPHPA YAVUNJA REKODI, MAKUSANYO YA MWAKA YAPATIKANA NDANI YA MIEZI MITATU

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru, akizungumza na waandishi wa habari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, mkutano huo umeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina. (Picha na Francis Dande)


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Afya ya Mimea, Dkt. Ben Nguwi, akifafanua jambo wakati wa mkutanmo huo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Viuatilifu, Oshingi Shilla, akijibu maswali ya Wahariri wa vyombo vya Habari wakati wa
mkutano wa kikao kazi baina ya Wahariri na Mamalaka hiyo kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.




Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Utekelezaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Yasin Sadick.

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 

MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imetangaza kuvunja rekodi ya Mapato ya Ndani, baada ya kukusanya kiasi cha Sh. Bilioni 6.1 katika kipindi cha miezi mitatu pekee.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Prof. Joseph Ndunguru, makusanyo hayo ni sawa na asilimia 95.2 ya makadirio ya makusanyo ya mwaka mzima kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani (own resources).

Akizungumza katika kikao kazi baina ya Wahariri na Mamalaka hiyo kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Profesa Nduguru alisema, fedha hizo zimepatikana katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Sepemba mwaka jana 2023.

Alisema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Mamlaka iliweka lengo la kukusanya kiasi cha Sh. Bilioni 6.4, lakini ndani ya miezi hiyo mitatu  hadi kufikia Septemba ikakusanya Bil. 6.1 na kubainisha kuwa matarajio ni kuvunja rekodi zaidi ifikapo mwisho wa mwaka.

“Ni wazi kwamba, hadi kufikia Mwisho wa Mwaka wa Fedha, TPHPA itakusanya zaidi ya asilima 100 ya makadirio hayo na hivyo kuongeza kiasi cha gawio lake kwa Serikali Kuu ambalo linakuwa ni asilima 15 ya pato letu.

"Hii maana yake ni nini? Kwa makadirio ya awali, tungeweza kutoa gawi la Serikali la Sh. Milioni 968, lakini kwa aina ya rekodi tuliyoweka ya makusanyo kwa Mwaka wa Fedha, maana yake gawio la Serikali Sasa litapanda na kufikia Sh. Bilioni 3.6," alisema Prof. Ndunguru

Akizungunzia mafanikio mengineyo, Prof. Ndunguru alibainisha kuwa katika Usimamizi wa Mimea, mamlaka yake ilifanya ukaguzi wa mazao na vipando ili kudhibiti visumbufu na kutoa leseni 39,230 za usafi wa mimea na kuruhusu usafirishaji kwenda nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Utekelezaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Yasin Sadick, aliishauri TPHPA kuwa macho kusimamia wafanyabishara wasio waadilifu wanaowauzia wakulima viuatilifu visivyo na ubora, jambo linalochangia kudidimiza sekta ya kilimo, ambayo ndio uti wa mgongo wa Taifa. 



No comments:

Post a Comment

Pages