March 08, 2024

UTT AMIS washerehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwafariji Wazee wenye mahitaji maalumu Msimbazi Center

 

Afisa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Doris Mlenge, akizungumza wakati wa kukabidhi vitu mbalimbali vilivyotolewa na Wafanyakazi Wanawake wa kampuni hiyo kwa ajili ya wazee wanaotunzwa katika kituo cha Msimbazi Center jijini Dar es Salaam. Misaada hiyo wameitoa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Sista Victoria akitoa shukrani zake baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi Wanawake wa UTT AMIS.

Wafanyakazi Wanawake wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS wakipokelewa na Sista Victoria baada ya kuwasili katika Kituo cha Kulelea Wazee wenye mahitaji maalumu cha Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

Afisa Mwandamizi wa UTT AMIS, Victoria Abuogo (katikati) akimkabidhi kisimbusi, mmoja wa wazee wanaotunzwa katika kituo hicho.

Sista Victoria akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa Wafanyakazi Wanawake wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS wakati walipotembelea makazi ya wazee eneo la Msimbazi Center jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2024 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.





No comments:

Post a Comment

Pages