April 23, 2024

Bajeti 2024/25 iwezeshe walimu kuhusu mtaala mpya

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI  imeshauriwa kutenga bajeti ya kutosha ili kuwapatia walimu wengi zaidi mafunzo ya Mtaala mpya kuwezesha utekelezaji wa ufanisi.


Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dk John Kalage ametoa ushauri huo, katika mkutano wa waandishi wa habari, wakati akitoa mapendekezo ya taasisi hiyo juu ya upangaji na utengaji wa bajeti ya sekta ya elimu ya Mwaka wa Fedha 2024/25.

"Mtaala mpya umekuja na majukumu ya ziada kwa walimu wa ngazi zote, msingi na sekondari. Ni wazi kuwa ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa mtaala mpya walimu wote wanapaswa kujengewa uwezo wa namna bora ya utekelezaji wake," amesema.

Pia ameshauri serikali kuwa na mpango maalum utakaoonyesha awamu ya utekelezaji wa mtaala mpya hadi kufikia shule zote.

"Serikali iainishe mpango maalum wa kifedha unaoonesha ni kiasi gani serikali imetenga kwa ajili ya kuandaa shule za sekondari kwa kila hatua katika maeneo ya ujenzi na ukarabati wa mindombinu inayohitajika katika utoaji wa elimu ya amali,

"Bajeti ya vifaa vya mafunzo ya amali hitajika na mpango wa gharama za kuajiri walimu wa elimu maalum ya amali na kujengea uwezo waliopo ili kusaidia utekelezaji wa mtaala mpya," amesema.

Dk Kalage amesema wanafahamu kuwa uamuzi wa serikali kutekeleza mtaala mpya kwa awamu ngazi ya sekondari, unatokana na hali ya maandalizi na uwekezaji mkubwa unaohitajika katika utoaji wa elimu kwa mchepuo wa amali.

Amesema HakiElimu inaona idadi hiyo ambayo ni asilimia 1.8 ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya shule za sekondari  nchini ambazo ni 5,289 ambapo shule 4,002 ni za umma na 1,287 ni za binafsi.


No comments:

Post a Comment

Pages