Washiriki wa Mkutano Maalum wa 53 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika
Mashariki uliofanyika tarehe 25 Aprili 2024 Makao Makuu ya Jumuiya
hiyo jijini Arusha katika picha ya kumbukumbu baada ya kumaliza mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu
Mkutano
Maalum wa 53 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki
umefanyika leo tarehe 25 Aprili 2024 Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini
Arusha.
Mkutano huo,
pamoja na masuala mengine umejadili na kupitisha Makadrio ya Bajeti ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.).
Viongozi
wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Naibu Waziri Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb.) na
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi.
Mkutano
huo umefanyika kufuatia kukamilika kwa kikao cha ngazi ya Makatibu
Wakuu kilichofanyika tarehe 24 Aprili 2024 ambacho kilitanguliwa na
kikao cha ngazi ya Wataalam cha tarehe 23 Aprili 2024.
No comments:
Post a Comment