April 03, 2024

CRDB, TFF wasaini mkataba wa Bil. 3.79

 

Benki ya CRDB imesaini makubaliano ya udhamini wa mashindano ya Federation Cup na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo kwa sasa yatajulikana kama CRDB Federation Cup.

Udhamini huu wenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.79 utakuwa wa miaka mitatu na nusu kuanzia hatua ya 16 bora msimu huu wa 2023/2024.

 

Makubaliano haya yanaifanya Benki ya CRDB kuwa mdhamini wa kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo ambayo yanashirikisha timu zaidi ya 100 kuanzia ngazi ya wilaya.

 

Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Aprili 2, 2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka TFF na Benki ya CRDB akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, AbdulMajidNsekela, Rais wa TFF, Wallece Karia, watendaji mbalimbali kutoka TFF, Wafanyakazi wa CRDB pamoja na waandishi wa habari.







No comments:

Post a Comment

Pages