Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
UKOSEFU wa elimu ya bima ya mali na vyombo mbalimbali kwa Watanzania, kumetajwa kuwa moja ya sababu ya watu wengi kushindwa kutambua umuhimu wake hali iyonachangia kwa kiasi kikubwa kupata hasara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali.
Amesema, moja ya shida iliyopo nchini ni elimu ya masuala ya bima ya mali mbalimbali kwa wananchi hali ambayo inasababisha watu wengi kushindwa kutambua umuhimu wake.
“Kukosekana kwa elimu ya bima za mali kwa watu wengi ndiko kumekuwa chanzo cha watu kushindwa kuwa na bima kutokana na kutotambua umuhimu wake hivyo unakuta watu wanamiliki nyumba, magari lakini hawana bima ya majanga kama vile moto na mengine hali ambayo inasababisha wengi wao kupata hasara”alisema
Amesema, kutokana na hali hiyo anaishauri serikali kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya masuala ya bima za mali ili kusaidia wananchi wengi ambao wamekuwa wakipata hasara ya mali zao kila yanapotokea majanga.
“Katika mataifa mengine bima ni jambo la lazima lakini leo hii hapa kwetu kutokana na watu kukosa elimu unakuta mtu anaweza kuingiza hata gari lake barabarani bila kuwa na bima na linapopata shida kama vile kupata ajali hakuna ambachopata zaidi ya hasara ya mali yake”alisema
Aidha, alisema ipo haja kwa serikali kuona umuhimu wa somo la bima kuanzia ngazi ya shule za msingi ili kuwajengea Watanzania uelewa wa umuhimu wa kuwa na bima za mali na vyombo mbalimbali.
“Mimi hadi namaliza shule sijawahi kuona sehemu kuna somo la bima hivyo ndiyo maana watu wengi wanapata shida hivyo juhudi zifanyike watu waoane umuhimu wa bima”amesema
Akizungumzia kuhusu huduma za bima zinazofuta sheria za kiislam alisema ni msaada kwa waumoni wa imani hiyo ambao wamekuwa wakishindwa kukata zile za kawaida kwa kuhofia mambo mbalimbali ikiwemo riba ambayo ni kinyume na imani zao.
“Bima hii inayofuata sheria za dini ya kiislamu inasaidia watu wenye imani hii kuwa na bima bila kuhofia kuharibu imani zao kutokana na zile zingine ambazo labda zimekuwa na masuala ya riba ndani yake au fedha zile kutumika katika mambo mengine ambayo ni kinyume na imani ya kiislam”alisema
Akizungumza kwa niaba ya Shekhe wa mkoa wa Dodoma Shekhe Ahmed Saidi, alisema kwa mujibu wa dini ya kiislam suala la riba ni haramu hivyo uwepo wa bima hiyo inayozingatia sheria ya dini za kiislamu kutasaidia waumini wengi kukatia mali zao bima ili kujiepusha na hasara zitokanazo na majanga mbalimbali.
No comments:
Post a Comment