Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema Serikali
itahakikisha elimu ya fedha inaingizwa kwenye mfumo rasmi wa elimu na
kuanza kufundishwa nchini.
Amebainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya siku tatu kuhusu uingizaji wa elimu ya fedha katika mitaala ya elimu ya juu iliyowakutanisha viongozi mbalimbali na taasisi za elimu ya juu nchini ambapo jambo hilo litatekelezwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Elimu, Seyansi na Teknolojia na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Amebainisha
kuwa elimu hiyo itatolewa katika vyuo vikuu lengo likiwa ni kuwawezesha
vijana kuwa na uwezo wa kuwa na nidhamu ya kusimamia fedha, kwamba
Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kujenga uelewa wa masuala ya
fedha kwa jamii.
“Wizara
tutahakikisha elimu ya fedha inafundishwa katika mfumo wa elimu nchini
hivyo twende kwa haraka kuhakikisha vijana ambao ni sehemu ya jamii
nchini wanakuwa na uelewa wa masuala ya fedha hivyo natarajia wakuu wa
vyuo mtabeba uelewa huo muhimu kwa vyuo vyetu nchini,” amesema
Kipanga.
Naibu
Waziri Kipanga amebainisha kuwa, BoT, itaendelea kusimama na vyuo na
taasisi za elimu na Wizara ya Elimu katika kuhakikisha dhana ya elimu
hiyo inakuwa endelevu na inafundishwa katika ngazi za jamii hata kwa
wale walio nje ya mfumo rasmi wa elimu nchini.
Ametumia
fursa hiyo kuviagiza Vyuo Vikuu nchini kushirikiana na BoT kufanya
tathmini ya utekelezaji wa mpango huo ili kuboresha mbinu na nyenzo za
kufikisha ujumbe huo kwa jamii.
Hivyo
amesema baada ya tathmini hiyo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
ipatiwe taarifa ili isaidie katika kufanya maamuzi kwani Serikali ya
Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria
kujenga uelewa wa masuala ya fedha kwa jamii.
Kwa
upande wake, Naibu Gavana wa BoT, Sauda Msemo amesema elimu ya fedha
inakuwa ni sehemu ya masomo, kwmaba somo hilo liingizwe kwenye mfumo ya
elimu msingi hadi vyuo vikuu.
Kwamba
Aprili mwaka jana, BoT iliwashirikisha wakuu wa taasisi za Elimu ya
Juu nchini, kwa uwakilishi wa wakuu wa vyuo vikuu pamoja na TCU na
NACTIVET kwa lengo la kukubaliana juu ya azma ya kufundisha somo la
elimu ya fedha ngazi ya elimu ya juu nchini.
“Hadi
hivi sasa taasisi tatu za elimu ya juu zimechukua hatua za kuingiza
somo la elimu ya fedha katika mitaala yao, hivyo warsha hii ni kuchochea
uwepo wa elimu ya fedha kwa vyuo vingi nchini kuendana na mabadiliko
ya mageuzi ya kiuchumi nchini,”amesema Msemo.
Msemo
ameeleza kwamba, takwimu ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022
inaonesha takribani watu asilimia 34.5 ni vijana walio na umri kati ya
miaka 15-35 hivyo ili kuleta tija na ufanisi katika masuala ya uchumi,
ujuzi na uzoefu wa masuala ya fedha ni moja ya sifa muhimu kufikia azma
hiyo.
Amesema
elimu hiyo ya fedha kwa Watanzania itachochea maendeleo kwa kuongeza
utumiaji rasmi wa huduma za fedha na kuwawezesha watu wengi kuwa na
uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kuendesha shughuli zao kwa
ufanisi na kukuza uchumi kwa ujumla.
Sauda
amesema elimu kwa vijana wa vyuo vikuu itawasaidia kuweka akiba,
kupanga bajeti na kufanya uamuzi wa masuala ya fedha kwa kuzingatia
viashiria hatarishi na kuelewa taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za
fedha ili kufanya maamuzi sahihi ya fedha ili waitawale.
"Tunatarajia
kujenga ‘displine’ ya fedha kupitia elimu ya fedha kwani watakuwa na
uwezo wa kutawala fedha sio fedha kuwatawala vijana hao,” ameongeza
Msemo.
Kadhalika
amesema BoT kwa kushirikiana na wadau wengine wa Baraza la Huduma
Jumuishi za Fedha, imetoa muongozo na mtaala wa elimu ya fedha kwa
wakufunzi ambao utatumika na taasisi za elimu ya juu kwa kuwafundisha
watoa huduma za elimu ya fedha kuwafikia wananchi wote walio nje mfumo
wa elimu.
“Tayari
tumeingia makubaliano na baadhi ya taasisi zaa elimu katika mtaala
huo wa kufunzi wa fedha na tulioingia nao makubaliano ni Chuo Kikuu cha
Iringa, Zanzibar, Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha
Benki Kuu ya Tanzania ,” ameseama.
Kwa
upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro
(SUA), Felix Adam amesema warsha hiyo ni muhimu kwake kwa sababu hayo
maeneo yanayojadiliwa yatawasaidia kuwapa elimu ya fedha wahitimu wao.
No comments:
Post a Comment