April 04, 2024

Inara Ceramic yampa Ubalozi Baba Levo kutangaza Tiles, awaomba Watanzania kununua bidhaa bora

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kampuni  ya Inara  Ceramic inayotengeneza Marumaru (Tiles) imempa ubalozi wa kuitangaza kampuni hiyo Msanii wa Muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina Baba Levo.
 


Akizungumza mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam, Baba Levo, amesema ameamua kujiunga na Inara Ceramic kutokana na kampuni hiyo kutokana ubora wao katika kutengeneza tiles kimataifa.

"Nina furaha kusaini mkataba wa miezi sita na baada ya hapo kama nitafanya vema nitaongezewa mkataba wa miaka mitatu," amesema.

Pia ameshawauri watu mbalimbali wanaofanya ujenzi kuhakikisha wanatumia tiles halisi kutoka kampuni hiyo kutoka India.

Wakati huo huo ameahidi kwa wateja watakaonunua tiles na zikiharibika ndani ya miezi sita  watarudishwa kiwandani kupata nyingine.

Amesisitiza kuwa atakwenda nchini India na ujumbe wa kampuni hiyo kuangalia jinsi tiles hizo zinavyotengenezwa hivyo atakaporejea ataendelea kuhakikisha anazitangaza wananchi wafahamu ubora wake.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo inauza tiles imara za kuweka ukutani, vyumbani na vyoo na kuwaomba watanzania wanunue kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zitakazodumu kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Manam Mody, amesema kuwa anaamini kujiunga Baba Levo naamini watafanya vema na kufika mbali.

Amesema kuwa wanatengeneza tiles zenye ubora zinazofaa kwa ujenzi wa nyumba za kisasa huku akiwaomba watanzania kuiunga mkono kampuni hiyo.


No comments:

Post a Comment

Pages