Na Magrethy Katengu
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Waumini wa Kanisa la The Word Reconciliation Ministries (WRM) kuendelea kufanya ibada za kwa ushirikiano kwa kumwomba Mungu ili awatimizie haja zao.
Akitoa salamu za Maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka Aprili 1, 2024 huku Kanisa hilo likiazimisha miaka 17 tangu kuanzishwa kwake kutoa huduma ya ibada Mhe Rais akiongea kwa njia ya Simu na Waamini hao amewashauri kuendelea kufuata mafundisho wanayofundishwa , kukaa kwa wema na kutunza Usalama .
"Nawatakia Pasaka njema na ibada njemaa Mungu azikubali ibada zetu na atimize haja zenu tunazozihiitaji hivyo nawasihi msiache kukusanyika kumwita kwa maombi "amesisitiza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi ya Watu Mhe Jerry Silaa ambaye amemwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassani katika Ibada hiyo amelipongeza kanisa hilo kutimiza maandiko kwa kulijali kundi kubwa la watoto kama ilivyoandikwa katika Mithali 22;6 kamaa ilivyoandikwa "Mlee mtoto katika njia impasayo hadi atakapokuwa mzee"
"Tunaishi kwenye kizazi ambacho pamoja na teknolojia kubwa ya mtandao baadhi ya makanisa nilienda nikakuta watu wazima hakuna hata mtoto wamewaacha nyumbani na vitu vya teknolojia hivyo nawasihi Tusichanganye mafanikio ya kiuchumi na malezi ya watoto"amesema Silaa
Naye Mwanzilishi wa Kanisa hilo Nabii Nicholaus Suguye amemshukuru sanaa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kusaidia kukamilisha usajili wa kanisa hilo hivyo amemuahidi kuwa watafanya huduma kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na kanisa hilo litakuwa kielelezo cha kuigwa.
Katika hatua nyingine Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani amemkabidhi Nabii Suguye zawadi iliyoletwa na Waziri Jerry Slaa na Kumkabidhi na Zawadi hiyoo pia na Nabii Suguye amemkabidhi Jerry Slaa Zawadi akampatie Rais Samia.
No comments:
Post a Comment