Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego akisalimiana na kwa furaha na Madereva Bajaji na Pikipiki wa Manispaa ya Singida baada ya kumaliza mkutano wake kwa mafanikio makubwa.
Bajaji zilizokuwa kwenye mkutano kwenye uwanja wa Bombadia mjini Singida.
Madereva Bajaji na Pikipiki wa Manispaa ya Singida wakicheza mbele ya Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego mara baada ya kufurahia kutatuliwa kwa kero zilizokuwa zinawasumbua kwa muda mrefu.
Madereva Bajaji na Bodaboda wa Manispaa ya Singida waliojitokeza katika viwanja vya Bombadia mjini Singida katika Mkutano wao na Mkuu wa mkoa wa Singida ili kutoa kero zinazowakabili.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego katika Mkutano wa kusikiliza kero zinazowakabili Madereva Bajaji na Pikipiki wa Manispaa ya Singida.
Mwenyekiti wa Dereva Bajaji na Bodaboda wa Manispaa ya Singida, Abdi Mitigo, akizungumza Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Singida akitoa kero mbalimbali zinazowakabili.
Mkuu wa mkoa wa Singida akizungumza na Madereva Bajaji na Pikipiki wa Manispaa ya Singida katika viwanja vya Bombadia mjini Singida kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amepiga marufuku madereva wa bajaji na pikipiki katika Manispaa ya Singida kulipa tozo yoyote bila kupewa risiti na mtu anayetoza tozo hizo.
Mkuu wa mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo (leo April 26 2024) kwenye Mkutano wake na Madereva wa Bodaboda na Bajaji katika Viwanja vya Bombadia kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili madereva hao na kuzitafutia fumbuzi.
Amesema ni jambo la aibu kwa Watendaji wanaokusanya mapato ya Serikali na kutotoa risiti wakati msisitizo mkubwa Serikali ni kuwa malipo ya aina yeyote lazima mnunuzi apewe risiti halali ili Serikali ipate mapato kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
“Haiwezekani kwa Serikali tuwe wa kwanza kutotoa risiti hilo halipo na haitawezekana tunataka haki bini haki, Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida ukakae na Mzabuni ili muweke utaribu wa kutoa risiti kama Serikali inavyoelekeza” Amesisitiza Halima Dendego.
Kuhusu mikopo ya Halmashauri, Mkuu huyo wa mkoa wa Singida amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida kukaa na Viongozi wa Madereva Pikipiki na Bajaji wa manispaa hiyo ili awasaidie kuanzisha Chama cha Kuweka na Kukopa – SACCOS - chama ambacho kitawasaidia kukopa fedha kwa ajili kununua vyombo vyao usafiri badala ya kuendesha vya watu hali ambayo itawasaidia kuboresha maisha yao.
Amesema kwa sasa Chama chao kina wanachama zaidi ya 4,000 hivyo wanaweza kukopeshwa na kurejesha mikopo yao kwa haraka kama Watendaji watawasaidia kuanzisha SACCOS yao.
“Wakianzisha SACCOS yao wapelekee milioni 200 waweze kukopeshana wao kwa wao kwa sababu wanajua na ulipaji wao utakuwa ni rahisi kuliko kukopesha makundi mengine ambayo hayaeleweki kwani watajiimarisha kiuchumi kwa kununua vyombo vyao vya usafiri kwa sababu kazi wanaiweza”
Naye, Mwenyekiti wa Madereva wa Bodaboda na Bajaji Manispaa ya Singida Abdi Mitigo amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Singida kwa kukutana nao na kutatua kero mbalimbali ambazo zilikuwa zinawanyima usingizi na kushindwa kufanya kazi ikiwemo tozo na ushuru.
No comments:
Post a Comment