Spika
wa Bunge, Dk Tulia Ackson (katikati) akifurahia jambo na Wajumbe wa
Bodi ya Benki ya NMB walipokutana kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa
NMB kwa Wabunge Dodoma. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya
NMB, Juma Kimori.
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson
(katikati) akiwa na watoto yatima wa kituo cha Zamzam kilichopo Miyuji
Jijini Dodoma mara baada ya kuwakabidhi masada wa chakula uliotolewa na
Benki ya NMB kwenye hafla ya futari iliyofanyika Bungeni jana ,wengine
kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NMB ,Dk Edwin Mhede na kushoto ni Afisa
Mkuu wa Benki ya NMB ,Juma Kimori.NA MWANDISHI WETU, DODOMA
WIKI
moja tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipoipo
ngeza Benki ya NMB kwa
jicho la huruma kwa Watoto Yatima, na kuzitaka Mamlaka za Serikali za
Mitaa na Taasisi za Fedha kujifunza kwao namna ya kuwafikia na
kuwasaidia wenye uhitaji, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson Mwansasu,
naye amekiri kuvutiwa na ibada hiyo.
Machi
26, Waziri Mkuu Majaliwa aliipongeza NMB kwa aina mpya ya ufuturishaji
wateja wao waliofunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, wadau na viongozi wa
Serikali, inayoenda sambamba na utoaji misaada kwa Watoto Yatima na
Wanaoishi kwenye Mazingira Magumu, na kutaka kuwepo mpango mkakati
uliobeba maono kama hayo.
Utaratibu
huo mpya wa ufuturishaji, ulianzia visiwani Zanzibar, ambako NMB
ilikabidhi misaada ya vyakula, mafuta ya kupikia, sukari, sabuni na
vifaa vingine kwa vituo vya Kidundo na Mazizini Orphanage, kisha
kuendelea ilipofuturisha jijini Dar es Salaam, ilikovisaidia vituo vya
Umrah, Tanzania Kwanza na Al Zam.
Akizungumza
wakati wa Iftar iliyojumuisha Viongozi wa Serikali, Wabunge wa Bunge la
Tanzania, wateja, wadau na Watoto Yatima wa Vituo vya Zam Zam na Darul
Maarifu vya jijini Dodoma, Spika, Dk. Tulia ambaye ni Rais wa Umoja wa
Mabunge Duniani, alisema NMB imefanya ibada kubwa kuwashika mkono Watoto
hao katika kipindi cha Ramadhan.
“Niwapongezea
kwa sadaka hii, ambayo mmenitaka mimi kuwakabidhi watoto hawa Afisa
Mkuu wa Fedha ameeleza hapa maeneo mbalimbali mlikopita kufuturisha na
kusaidia jamii ya wenye uhitaji, viongozi wa serikali na wateja wenu,
tunawapongeza kwa sababu mmeenda kuwafuturisha wapiga kura wetu huko.
“Tunaithamini
sadaka hii, tunawapongeza NMB kwa kazi nzuri, na hii ni kwa niaba ya
wote waliofuturu hapa na ambao hawawezi kupata fursa ya kuongea, naomba
mfahamu tu kuwa tunaheshimu sana sadaka hii mliyoitoa leo hapa na kule
kote mlikofuturisha.
“Tunawashukuru
sana NMB, kwakweli mnafanya vizuri na tunawapongeza sana sana, kwa kuwa
hii ni taasisi ya kifedha, inayofanya kazi za maendeleo. Tunawapongeza
kwa mchango mkubwa wa maendeleo ya taifa mnaotoa kwa Serikali ya Awamu
ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan,” alibainisha Spika, Dk. Tulia.
Akinukuu
Qur ani Tukufu Surah ya 99 (Az Zalzalah), aya ya saba hadi ya nane –
(inayosema; Basi yule mwenye kutenda wema mdogo mfano wa mdudu chungu,
atalipwa na mwenye kutenda uovu/ubaya mdogo mfano wa sisimizi,
atalipwa), Spika Tulia aliitabiria mafanikio makubwa NMB kwa ukubwa wa
ibada za kijamii inazofanya.
“Ni
matumaini yetu kuwa kwa kazi nzuri mnayofanya, ikiwemo kujali na
kuthamini haya makundi maalum, mafanikio yenu yatakuwa makubwa zaidi na
miaka ijayo tutashuhudia hafla hizi majimboni ama mikoani, kwa sababu
Allah atakuongezeeni mafanikio kutokana na ibada zenu za kuwajali watoto
hawa.
Awali, Afisa Mkuu
wa Fedha wa NMB, Juma Kimori, ambaye alimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu
wa benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna, alisema ufuturisha wateja, waumini na
wadau wao umekuiwa wa muda mrefu, lakini mtazamo chanya kwa jamii
ukawasukuma kufikiria kufanya kitu kwa makundi ya wenye uhitaji.
“Kila
mwaka huwa tunafanya hafla hizi, lengo likiwa kudumisha ukaribu na
kustawisha mahusiano mem ana jamii inayotuunga mkono, lakini namna ya
kipekee mwaka huu tumekuwa tukialika watoto kutoka katika vituo vya
wenye mahitaji maalum na kuwasaidia, leo tukiwa na takribani watoto 100
kutoka vituo vya hapa Dodoma.
“Tunaamini
kwamba hii ni fursa ya watoto hawa kujifunza na kuendelea kuhamasika
kutenda mema na kuwa wakarimu kwa jamii. Ndio kusema leo hatutoishia tu
kufuturisha, bali tutawasaidia watoto wa Vituo vilivyo chini ya Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), vya Zam Zam na Darul Maarifu vya
hapa Dodoma,” alibainisha Kimori.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede, alimshukuru Spika Tulia kwa
kuhudhuria hafla hiyo na kwa niaba ya Bodi, wanamshukuru yeye kutenga
muda wa kujumuika nao, huku akisema NMB na Bodi kwa niaba ya wanahisa
wanawashukuru pia waalikwa wote na ujio wao ni ishara kwamba wana
mashirikiano mema na wadau.
“Na
kwenye mashirikiano mema, kuna kuelimishana, kukosoana ili kujengana
kwa nia ya kufanya vizuri zaidi na katika mkutano huu wa ibada,
hatutaacha kupokea maoni na mrejesho kutoka kwenu ili kutusaidia tuweze
kuimarisha oparesheni zetu na huduma kwa wananchi na sekta
tunazozihudumia kila siku.
“Ukiachana
na ukweli kwamba hii ni ibada, lakini kwanini tunakutana? Kitabu
Kitukufu cha Qur ani kinatuasa na kutuhimiza umuhimu wa kukutana na
kukumbushana, kwani inaaminika kwamba katika kukumbushana, ndiko
tunakoweza kujengana vizuri kabisa. Kwa hiyo kusanyiko hili ni la
Kimungu na lina baraka zote,” alifafanua Dk. Mhede.
No comments:
Post a Comment