April 15, 2024

TBS YAJIDHATITI UJENZI WA MAABARA KANDA YA ZIWA NA KASKAZINI


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) Dkt. Athuman Ngenya, akizungumza wakati wa kikao kazi cha Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR) na kufanyika jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akizungumza katika mkutano huo.

 

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim (kushoto) akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga.

Baadhi ya Wahariri na Waandishi wa Habari wakiwa katika mkutano huo.
Meneja Udhibiti Ubora wa Bidhaa ziingiazo na zinazotoka nchini, Gervas Kaisi, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga, akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari.
Mhariri wa Kituo cha Luninga cha Channel Ten, Khamis Mkotya, akiuliza swali wakati wa mkutano huo. 

Mkurugenzi wa TBS Dk. Athuman Ngenya (kulia) akimsikiliza Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Salim Said Salim (kushoto) wakati wa kikao kazi cha Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR) na kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga.

 

Na Mwandishi Wetu


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuanza ujenzi wa maabara ya kisasa katika kanda ya Ziwa (Mwanza) na kanda ya kaskazini (Arusha). Maabara ya kanda ya ziwa inatarajiwa kuhudumia mikoa sita (6) ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu.

 

Akizungumza na waaandishi wa habari leo Mkurugenzi wa TBS Dkt. Athuman Ngenya amesema maabara ya kanda ya Kaskazini inatarajiwa kuhudumia mikoa minne (4) ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara.


“Shirika linatarajia kuanza ujenzi wa maabara ya kisasa katika kanda ya Ziwa (Mwanza) na kanda ya kaskazini (Arusha). Maabara ya kanda ya ziwa inatarajiwa kuhudumia mikoa sita (6) ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu. Aidha, maabara ya kanda ya Kaskazini inatarajiwa kuhudumia mikoa minne (4) ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara.


Katika hatua nyingine amesema “Shirika limetengeneza mifumo ya kielektroniki inayotumika kutoa huduma zake. Uanzishwaji wa mifumo ya kielektroniki imewezesha wateja kupata huduma za TBS popote walipo kwa wepesi na haraka hivyo kupunguza gharama kwa wateja.


“Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya viwango 1,721 vya kitaifa viliandaliwa sawa na asilimia 101.2 ya lengo la kuandaa viwango 1,700. Viwango hivyo viliandaliwa katika nyanja mbalimbali.TBS imeshiriki katika uandaaji wa viwango vya kibiashara vya Afrika Mashariki na Afrika nzima.

Kuhusu Utoaji wa leseni za Alama ya Ubora amesema “Serikali kwa kupitia TBS imekuwa ikitenga zaidi ya milioni 250 kwa dhumuni la kuhudumia wajasiriamali wadogo bila ya malipo yoyote.


“Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya leseni za ubora wa bidhaa 2,106 zilitolewa kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000. Kati ya leseni hizo, jumla ya leseni 1,051 zilitolewa bure na kwa Wajasiriamali wadogo.


“Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya wadau 5,789 kutoka mikoa mbalimbali nchini walipewa mafunzo hayo. TBS imeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo (MSEs) na wazalishaji ili kuwawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango vya ubora na usalama na hatimaye kukidhi ushindani wa masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.


Aidha kuhusu ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi amesema kuwa “TBS hudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje kwa kutumia mfumo wa Pre-Shipment Verification of Conformity to Standards (PVoC) pamoja na kufanya ukaguzi pindi bidhaa zinapowasili nchini (Destination Inspection).


“Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya shehena 100,851 kabla hazijaingizwa nchini sawa na asilimia 99 ya lengo la kukagua shehena 102,083. Pia, jumla ya bidhaa 151,570 kutoka nje ya nchi zilikaguliwa baada ya kufika nchini sawa na asilimia 77 ya lengo la kukagua bidhaa 197,417.”amesema.

TBS hudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje kwa kutumia mfumo wa ‘Pre-Shipment Verification of Conformity to Standards (PVoC)’ pamoja na kufanya ukaguzi pindi bidhaa zinapowasili nchini (Destination Inspection).


Kwa kipindi cha miaka mitatu, jumla ya shehena 100,851 kabla hazijaingizwa nchini sawa na asilimia 99 ya lengo la kukagua shehena 102,083. Pia, jumla ya bidhaa 151,570 kutoka nje ya nchi zilikaguliwa baada ya kufika nchini sawa na asilimia 77 ya lengo la kukagua bidhaa 197,417.


Jukumu Kuu la TBS ni kuratibu uandaaji wa viwango na kusimamia utekelezaji wake (shughuli za utayarishaji wa viwango na udhibiti wa ubora wa bidhaa zote pamoja na kusimamia usalama wa  bidhaa za chakula na vipodozi).

No comments:

Post a Comment

Pages