Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo, akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR).
Baadhi ya Wahariri wakiwa katika kikao kazi hicho.
Mkurugenzi wa Masoko Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Deo Kwiyuka, akizungumza wakati wa kikao kazi cha Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR).
Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Regina Semakafu, akifafanua jambo wa kikao kazi cha Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na Wahariri wa Vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR).
Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akizungumza katika mkutano huo.Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Nevilli Meena, akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR).
Na Mwandishi Wetu
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika kipindi cha robo ya mwaka 2024 imetengeneza faida ya shilingi Bilioni 10.7 baada ya kodi. Faida hiyo ni ongezeko la asilimia 529 ikilinganishwa na shilingi Bilioni 1.7 kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2023, huku ikitarajia kukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 40.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo, Adam Mihayo amesema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari. amesema faida kabla ya kodi ilikuwa shilingi Bilioni 13.6 kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu ambayo ni sawa na asilimia 353 ukilinganisha na shilingi Bilioni tatu.
Mapato ya Benki ya Biashara Tanzania kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2024 yamefikia shilingi Bilioni 56.8 kutoka shilingi Bilioni 43.7 Kwa kipindi kama hicho mwaka 2023.
“Ninajivunia kuwatangazia utendaji wetu wa kipekee katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2024. Ukuaji mkubwa huu unasukumwa na dhamira yetu ya dhati na kujizatiti kwetu katika ufanisi ili kumridhisha mteja. Sisi ni benki ambayo inachukua muda wake kuwasikiliza wateja wetu na kuweka juhudi katika kuelewa mahitaji yao.”
Ameendelea kusema, “kwa ongezeko hili la mapato kwa asilimia 30 tumedhihirisha kwa mara nyingine tena ujasiri wetu, na uwezo wetu wa kulikabili soko linalokua kwa kasi. Imani ya wateja wetu kwetu bado ni imara kama inavyothibitishwa na ongezeko la amana ya wateja.
Vile vile, dhamira yetu katika kuimarisha ukuaji wa uchumi inadhihirika wazi katika ongezeko la mikopo kwa wateja wetu. Tukiendelea na safari hii ya mafanikio, tunajizatiti kuwafikishia watu ubunifu wa kifedha na kuchangia katika ustawi wa watu wetu na Taifa letu kwa ujumla.”
“Tumejizatiti kuendeleza jitihada katika kutekeleza mkakati wetu ambao unazingatia ufanisi wa uendeshaji, na kuendelea kupunguza gharama zetu kwa uwiano wa mapato licha ya kuongezeka kwa kipindi hiki."amesema Mihayo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Nevilli Meena, amesema benki hiyo inapaswa kutoa elimu kwa waandishi wa habari hasa waandishi wa habari za biashara za Kiswahili ili kuweza kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii juu ya nini kinafanyika ndani ya taasisi hiyo na faida zake.
“Habari za Biashara mara nyingi zinagusa watu wengi ambao wanafahamu kiingereza, naomba niwasilishe ombi kwenu kuelekea miaka 100 ya benki hii, ifikirieni sekta ya habari kwa maana ya waandishi wa habari za biashara ambao wataweza kuandika vizuri habari za Kiswahili zinazosomeka na kueleweka kwa wasomaji wa kawaida. Watu wakajua hapa TCB kuna huduma ya mikopo kwa kusoma na kuelewa.
“Ikiwa mtafanikiwa wafundishwe kuandika vizuri habari zinazosomeka ambazo zitasaidia watu kusoma na kuelewa. Sisi jukwaa la wahariri tupo tunaweza kushirikiana na taasisi nyingine za habari kuangalia waandishi ambao wanaandika habari za biashara hata kama ni kwenye mitandao ya kijamii watu wana simu janja wanasoma na kuangalia.”
Meena amewataka waandishi kuacha kuandika kitu ambacho hawakijui bali waulize wahusika ili kuweza kufukisha ujumbe uliokusudiwa kwa wananchi.
Kuhusu Tanzania Commercial Bank (TCB) Ni taasisi ya kifedha ya Tanzania, ambayo imejikita katika kutoka suluhisho la kifedha. Ikiwa na historia pana na uwajibikaji katika kumridhisha mteja, TCB Benki imedhamiria kuwa benki pendwa zaidi na rafiki kwa wateja nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment