April 19, 2024

ZIARA YA RAIS SAMIA ANKARA -UTURUKI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakiangalia album ya picha za matukio ya Ziara Rasmi aliyoifanya katika Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024. 
Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu Kulliye Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima mbele ya kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na kwa upande wa Uturuki Rais wa Baraza la Elimu Profesa Dkt. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Uturuki tarehe 18 Aprili, 2024.

Picha namba 14. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Lela Muhamed Mussa pamoja na Rais wa Baraza la Utalii la Jamhuri ya Uturuki Abdullah Eren wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika Elimu ya Juu tarehe 18 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wa utiaji saini Hati za makubaliano kati ya Ofisi ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki iliyowakilishwa na Zeynel Kılınç, Makamu wa Rais wa Ofisi ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki na kwa upande wa Tanzania iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Gilead Teri tarehe 18 Aprili, 2024.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages