May 02, 2024

LPG yapongeza Serikali kwa juhudi ya kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

Chama Wafanyabiashara  Waagizani  na Wasambazaji wa gesi ya kupikia Majumbani  LPG Kimeipongeza Serikali kwa juhudi wanayoifanya kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi wake wenye kipato cha chini ikiwemo Mama na baba lishe, ili kusaidia kuondokana na matumizi ya nishati chafu ikiwemo kuni na mkaa.



Ameyasema hayo leo May 1, 2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara wasambazaji na waagizaji  gesi ya kupikia ya majumbani Amosi Mwansumbue ambapo amebainisha pamoja na serikali kusaidia hilo lazima wanaopokea mitungi wanapotumia wawe wanaweka bajeti mara baada ya gesi kuisha siyo  kuwekwa ndani kwani kufanya hivyo ni kuzimisha ndoto za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani  na wadau wanaounga jitihada hizo za kuacha matumizi ya nishati chafu.

Sambamba na hayo amesema baada ya mtu kuanza kutumia gesi lazima awe na maandalizi ya kifikra  kuweka bajeti akitolea mfano wakati simu zilipoingia watu waliona ni gharama kubwa kumiliki kwa matumizi lakini walipoanza kuelimika wakanunua hadi vijijini tena simu za bei kubwa na matumizi lazima vocha hivyo kwa kuwa waligundua inawapunguzia gharama ya kutafuta huduma hivyo simu ikiwa haina vocha mtu anahangaika mpaka  anaweka vocha hivyo hata suala la mtaumizi ya gesi yakupikia lazima kutengewa bajeti ili inapoisha mtungi usiwekwe ndani bali uendelee kujazwa na kutumika  .

" Kiukweli hiii Programu  ya serikali kwa kushirikiana na Rea Wabunge chini  ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani  ya kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi wa hali ya chini ni ya kipekee sana kwani taasisi za kifedha  za kimataifa wamejitolea kuunga mkono Tanzania huku na sisi Wanachama wetu tumeshiriki kwa kutoa  gharama ya theluthi moja mitungi kwa bei ya chini ili kila mmoja apate hivyo  hatutegemei kabisa baada ya mtungi kuisha gesi watu wataenda kuiweka na kurudi kwenye nishati chafu nawasihi wafikiri kabla ya kutenda " amesema Amosi

Sanjari na hayo amesbainisha kuwa Mtungi wa gesi usiporudi ni hasara  akitolea mfano sawa na basi la abiria analipa nauli ili asafiri hivyo  hivyo mtungi ni gari kwa biashara yao lazima uuze gesi kwa kutumia mtungi na  mtungi usiporudi kwa kujazwa gesi nyingine wao wanapata hasara kutokana na mitungi haizalishi  mauzo yanayohitajika hivyo kupelekea gharama ya uwekezaji kuwa juu wawekezaji wanapotaka kuja Tanzania kuwekeza katika sekta hiyo wakiliona tatizo hilo watakimbia na ukiangalia wanaoagiza gesi nje ya nchi na kuishambaza ni wachache hivyo wanawaomba watu wasiweke mitungi muda mrefu ndani .


Mkurugenzi amesema hivi karibuni ameona serikali ikizuia na kukamata mikaa inayotoka mikoani hivyo kusababisha gharama za Mkaa kupanda hasa mkoa wa Dar es salaam gunia moja kuuzwa elfu sabini hivyo kutokana na hali hiyo baadhi ya watu wenye familia kuanzia watu watano wamejikuta matumizi ya mkaa  kuwa ni gharama kubwa  na kuonekana mtungi wa gesi wa kg 6 kuuzwa kuanzia  23000hadi 24000 kutegemeana na mahali hivyo ikaongeza kasi kwa watumiaji gesi kwani  kuwa na gharama ya chini hivyo serikali ikiendelea na ufuatiliaji kila mahali nchi zima Lengo la hadi kufikia 2033 angalau asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati mbadala.

Amosi akizungumzia juu ya Tunzo ya kimataifa ya Afrika aliyotunukiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia amesema kuwa hiyo imedhihirisha mfano wa kuigwa na  mwezi ujao anatarajiwa kuhudhuria Mkutano huko Ufaransa Parisi Unaowakutanisha wadau wa nishati na yeye  kuwa mwenyekiti mweza katika mkutano huo na  wanakwenda kujadili namna ya kuendeleza nishati safi hasa kumwinua mwanamke.

Mkurugenzi Amosi amesema  Mwaka huu wamenamshukuru sana Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko kwa mpango wake wa kushirikisha sekta binafsi kabla ya kwenda kusoma bajeti Bungeni ni kitu kipya sana kwao cha kipekee kwani aliwaalika Dodoma ili awapatie ufafanuzi na kutoa maoni yao kabla hajawasilisha bajeti ni jambo jema kwani haijawahi kutokea kipindi cha miaka ya nyuma walikuwa wanashangaa tu bajeti inasomwa pasipokushirikishwa lakini mwaka huu Waziri huyo alichukua vipaumbele vyao na baadhi ya maeneo yalifanyiwa marekebisho.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Benoit Araman amesema lengo la kugawa mitungi  ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za za Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kuona matumizi ya nishati safi yanapewa kipaumbele.hivyo imekuwa ikigawa mitungi bure kwa makundi ikiwemo Mama lishe watumishi wa afya

"Tumekuwa tukigawa mitungi ya gesi na majiko yake bure kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya baba na Mama Lishe,watumishi wa sekta ya afya na wajasiriamali. kama ambavyo wamekuwa wakiahidi siku zote wataendelea na kampeni hiyo kadri ya uwezo wao lengo ni kuona wanafikiwa wananchi wengi zaidi  hadi sasa Oryx Ges Tanzania mpaka sasa tumeshatoa mitungi ya gesi zaidi ya 33,000 maeneo mbalimbali nchini na kiasi cha Sh  bilioni 1.5

Aidha Wanachama hao wanaishukuru serikali kwa kuwaondolea kodi  na baadhi ya vifaa LPG hivyo wanaomba kuboreshewa miundombinu ya Bandari hasa pakupokelea gesi ili kuweza kuruhusu meli kubwa zaidi na  wanapojenga Maghala makubwa yaendane na uwezo wa bandari kupokea meli kubwa zinazoleta kiwango kikubwa cha gesi kwa wakati mmoja kwani itachangia bei ya gesi kuwa nafuu.

 



No comments:

Post a Comment

Pages