Mkuu wa Wilaya ya Magu , akipokea zawadi ya kombe la mshindi wa jumla mashindano ya ya umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITAMSHUMTA) kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza zilizoshiriki mashindano hayo leo Ijumaa Mei 31,2023.
Halmashauri
ya Wilaya ya Magu imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika Mashindano ya
umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania
(UMITASHUMTA) kwa kuchukua vikombe 13 katika fani za mpira wa kikapu
wavulana na wasichana, riadha , kwaya, ngoma, mpira wa miguu wavulana,
handball , usafi na nidhamu na kombe la mshindi wa jumla katika
Halmashauri zote za mkoa wa mwanza zilizoshiriki mashindano hayo.
Akitangaza
matokeo hayo mbele ya mkuu wa Wilaya Afisa utamaduni wa Wilaya ya Magu,
Peter Mujaya amesema magu imebeba vikombe 13 katika fani ya mpira wa
kikapu wavulana na wasichana nafasi ya kwanza, mpira wa mikono wavulana
nafasi ya 2, na wasichana nafasi ya tatu, riadha wasichana nafasi ya 1
na wavulana nafasi ya 3, kwaya nafasi ya 1, ngoma nafasi ya 2 , muziki
nafasi ya 3, mpira wa miguu nafasi ya 3, usafi na nidhamu nafasi ya 1,
mpira wa wavu nafasi ya 3 pamoja na kombe la mshindi wa jumla kwa mkoa
wa mwanza.
Akizungumza wakati akipokea vikombe hivyo leo Mkuu wa
Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari amewapongeza vijana kufanya vizuri
kwa katika mashindano hayo na akasisitiza kuongeza bidii na kufanya
vizuri zaidi katika mashindano ya Kitaifa.
Aidha DC Nassari
ametoa rai kwa wanafunzi hao kutumia ushindi huo katika kuongeza juhudi
na bidii katika taaluma na kufanya vizuri katika masomo yao ili kufikia
malengo yao na kuifanya wilaya ifanye vizuri katika taaluma.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani
ametoa pongezi kwa wote waliofanikisha ushindi na kuwataka wafanye
vizuri zaidi kwa mashindano mengine hapo mwakani.
Vijana 26
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Magu wameteuliwa kuunda timu ya mkoa
itakayoshiriki mashindano ya UMITASHUMTA taifa yatakayofanyika mwezi
Juni Mkoani Tabora.
No comments:
Post a Comment