May 10, 2024

MILIKI NA UBUNIFU NI CHANZO CHA KUSUKUMA MAENDELEO YA NCHI KIUCHUMI

Na Magrethy Katengu--Dar es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote wa sekta binafsi na Umma kwa kuhakikisha kunakuwepo na mifumo thabiti ya kusimamia Miliki Ubunifu nchini ili ili kusaidia kupata suluhisho la changamoto zinazoikumba jamii ikiwemo za kiuchumi.


 Ameyasema hayo leo May 9,2024 Jijini Dar es salaam  Naibu  Waziri wa Utamaduni Sanaa  na Michezo Hamis Mwinjuma aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji katika Maadhimisho ya  ya Miliki Ubunifu  ya Dunia ambapo huadhimishwa Aprili 26 lakini Tanzania imefanya siku hiyo muhimu May 9 kwa kukutanisha taasisi binafsi na serikali kufanya mjadala wa pamoja na kusainia saini za hati za makubaliano na BRELA.

 Naibu Waziri Mwinjuma amesisitiza kuwa Maadhimisho hayo ni muhimu sana kwani yanawaleta pamoja kujadili fursa zilizopo za Ubunifu na changamoto katika ngazi ya kitaifa kikanda na kimataifa hivyo ni budi kufahamu kuwa Dunia imebadilika na sasa ili kupata maendeleo ya haraka lazima kuwepo Ubunifu na tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto na kuleta usuluhishi wa matatizo ya kijamii

"Niwapongeze sanaa kwa ushiriki wenu mkubwa nyinyi ni wadau muhimu sana  hamjapoteza siku yenu bure kwani mtabadilishana uzoefu taasisi kwa taasisi na na kujipatia maarifa mapya na kila mmoja atakaporudi mwakani tena atakuja na bunifu nzuri " amesema Naibu Waziri

Waziri amebainisha kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira bora na wezeshi na hivyo kupitia bunifu na tafiti zenu Taifa limeendelea kuimarika kuimarika na kufikia uchumi wa kati

Pia Waziri amesema.serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha sera ya taifa ya miliki bunifu itakayotoa mwongozo thabiti katika kusimamia masuala hayo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Geofrey Nyaisa, amesema bado kuna changamoto ya uelewa wa masuala ya miliki ubunifu na kwamba wameendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia vyuo, wafanyabiashara na wajasiriamali ili kuhakikisha bunifu zinalindwa na kutumika katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hata hivyo Mkurugenzi Brela amesema kwa  mujibu wa Nyaisa, mwaka 2023/2024 wametoa elimu  Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM), Chuo Kikuu za Mzumbe, vyuo vya Veta na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO). Pia wametoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Geita, Njombe.

Aidha Brela  wanatoa ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili katika miliki ubunifu kwa kushirikiana na Shirika la Miliki Bunifu Kanda ya Afrika kwa kuongeza wataalam katika maeneo ambapo  mpaka sasa wanafunzi 13 wamenufaika na fursa hiyo.

Sambamba na hayo katika hafla hiyo Brela imeingia makubaliano ya ushirikiano na TIA, Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ili kuimarisha shughuli za miliki


Mtendaji Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru, amesema makubaliano hayo yataongeza tija na kuimarisha usalama wa afya ya binadamu na mazingira.

“Tulibaini changamoto mifumo ilikuwa haisomani, kila taasisi ilikuwa inafanya kazi kila taasisi kivyakevyake hivyo, makubaliano haya yatasaidia kutatua changamoto na mifumo itasomana na ameahidi kuwa wataandaa mafunzo ya pamoja kusaidia  wafanyabiashara wanaosajili viuatilifu wawe tayari wamejisajili Brela,” amesema Profesa Ndunguru.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Vedastus Timothy, ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira yanayochochea matumizi ya shughuli za ubunifu nchini kwani zina mchango mkubwa katika kutatua changamoto za sekta mbalimbali.

Siku ya Miliki UBunifu Duniania huadhimisha Aprili 26 kila mwaka lakini Tanzania imeadhimishwa leo Maya 9 kwa sababu ya sherehe za Muungano hivyo  Kaulimbiu ya mwaka huu inasema ‘Miliki ubunifu na malengo ya maendeleo endelevu; kujenga mustakabali wa pamoja kwa kutumia ubunifu’.





No comments:

Post a Comment

Pages