Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Mobhare Matinyi amesema Serikali itaendelea kuheshimu na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini ikiwa ni pamoja na kusisitiza uwahibikaji utakaowezesha chaguzi zetu kuwa wazi,jumuishi na zenye kuheshimika.
" Kwa pamoja tunaweza kujenga demokrasia imara zaidi ambapo vyombo vya habari vinakua kichocheo cha mabadiliko chanya na maendeleo ya kijamii" amesema Matinyi.
"Tunaishi katika nyakati ambazo habari zinapatikana na kusambaa kwa urahisi na kwa kasi ya juu sana na hivyo kukazimu umakini na usahihi wa kiwango cha juu hivyohivyo usambazaji wa habari za uongo, upotoshaji na habari zinazosababisha uhasama unaoweza kudhoofisha taswira ya uchaguzi zetu na kuharibu imani ya umma kwa mantiki hii ni jukumu la kila mdau pamoja vyombo vya habari kudumisha viwango vya juu vya weledi kufuatia miongozo ya maadili na kukuza uandishi wa habari unaowajibika amesema Matinyi.
"Nalipongeza Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa jitihada zake katika kuendeleza weledi, maadilina uwajibikaji katika tasnia ya habari kwani majukumu ya MCT ni kuhakikisha tunakua na uandishi wa habari wenye viwango bora.
Aidha tunahamasisha uhuru wa vyombo vya habari na wanatetea haki za waandishi wa habari ambayo ni majukumu muhimu katika demokrasia inayostawi ,hivyo wanapaswa kupongezwa"
amesema Matinyi.
Amesema kuwa vyombo vya haba vina wajibu mkubwa na muhimu katika jamii yoyote yenye demokrasia kwa sababu mijadala mbalimbali kwenye umma.
Tunapokaribia katika mchakato wa uchaguzi jukuku la vyombo vya habari linakua ni muhimu zaidi kwa kupitia majukwaa yenu ndipo wananchi wanapopata habari habari ikowa ni pamoja na kuelimishwa jinsi ya kusiriki katika chaguzi na hivyo kupata na kutumia fursa ya kufanya maamuzi yenye manufaa kwao.
No comments:
Post a Comment