June 20, 2024

DC KISARAWE AUNGANA NA WATAALAM KUJIONEA MWENENDO MRADI WA VISEGESE

NA VICTOR MASANGU, KISARAWE

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti  amefanya kikao kazi na   wataalam wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyi pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Mradi wa viwanja vya Uwekezaji wa Viwanda.

Mkuu wa Wilaya hiyo pia katika kikao hicho ameweza kuongozana na  Viongozi mbali mbali  wa Halmashauri ya Kisarawe pamoja na Timu ya Watalaam na kupata fursa ya kutembelea  eneo la Mradi wa upangaji wa Upimaji wa Eneo la Viwanda lililopo Visegese kata ya Kazimzumbwi.

Mhe.Magoti alisema kwamba mradi wa Upangaji wa upimaji  ulibuniwa kwa ajili ya kutenga viwanja kwa ajili ya Viwanda na Maeneo mbali mbali  ya Makazi ya watu.

Magoti alifafanua kuwa utekelezaji wa Mradi huo ulianza kutekelezwa.mnamo  mwaka 2014 na kufanikiwa kuzalisha Viwanja 291 hivyo eneo hilo litakuwa Maalum kwa ajili ya Viwanda vya aina mbali mbali.

"Utekelezaji wa Mradi huu ulifanyika kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Wananchi wenye Maeneo katika Eneo lililopendekezwa kwa lengo la uwelezaji huo,"alisema Mhe.Magoti

Mkuu huyo alieleza kuwa muda  si Mrefu Wananchi wote  wenye nia yakutaka kuwekeza nakujenga Viwanda Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa pwani karibuni sana sana.Huduma za Maji zipo na barabara tupo mbioni kuzishughulikia ili kupanua wigo wa usafirishaji.

Pia alifafanua kwamba Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan  anapenda kuona Wananchi wake wanapata kipato kikubwa na kuinua uchumi wa kimaendeleo yenye kuleta mabadiliko na kuboresha  maisha yao kwa ujumla.



No comments:

Post a Comment

Pages