Baada ya miaka 10 Kampuni ya Saruji ya Mbeya inayojulikana na chapa yake ya Tembo ambayo pia ni kampuni tanzu ya Amsons,imetoa gawio la Sh 3 bilioni kwa Serikali. Mafanikio haya ni matokeo ya mabadiliko yaliyofanywa na wanahisa hususan Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya kutengeneza mazuri na rafiki kwa wawekezaji kupitia falsafa yake ya 4Rs.
Tunajivunia mafanikio haya kwasababu kwa kipindi cha miaka 10 kampuni hii haikuwa kutoa gawio kwa wanahisa wake, ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 2014 haya ni mabadiliko ya kuungwa mkono alisema Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu wakati wa kikao kifupi cha wanahisa na menejimenti kilichofanyika jana kiwandani hapo.
Jambo la pili la kujivunia ni kampuni hii kuwa kampuni ya kwanza kumilikiwa na kuendeshwa na wazawa ikiwa ni uwezeshaji uliofanywa na serikali yetu alisisitiza Mchechu
Serikali kama mmoja wa wanahisa katika kampuni hiyo ikwa na umiliki wa asilimia 25 na kupitia kwa Msajili wa Hazina imepokea kiasi cha Sh 3 bilioni na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wenye hisa asilimia 10 umepokea Sh 1.2 bilioni kama gawio.
Pia,ikumbukwe kwamba, umiliki wa hisa nyingi za asilimia 65 ndani ya kampuni ya Saruji Mbeya, zilichukuliwa na makampuni ya Amsons ya Tanzania kutoka kwa Holcim ya Uswisi.
Hata hivyo,wanahisa walitembelea kiwanda cha kuzalisha saruji kilichopo Mbeya Mei 31,2024 na walisisitiza kuendelea kuunga mkono na kuhakikisha kuna ukuaji endelevu kwa miaka ijayo kwa faida ya wadau wote na kuongeza thamani kwa wanahisa wake.
Akizungumza na Wafanyakazi kiwandani hapo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alisema uwepo wa kiwanda hiki ni maono ya Mwalimu Nyerere miaka ya 1978 hivyo tunapaswa kuyalinda maono haya kwa manufaa ya vizazi vyetu lakini ili tufanye vizuri zaidi tunaitaji kupunguza gharama za uzalishaji ili kukuza faida yetu
Mbeya Cement Company Limited (MCCL) ilianzishwa nchini Tanzania chini ya Sheria ya Makampuni, 2002 kama kampuni binafsi iliyoko Songwe, Mbeya ambayo inajishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa saruji.
No comments:
Post a Comment