July 25, 2024

RC CHALAMILA; VYOMBO VYA HABARI PUNGUZENI KURIPOTI HABARU ZINAZOLETA TAHARUKI

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amevitaka vyombo vya habari vinavyoripoti taarifa juu ya suala la uibukaji utekaji watoto kupunguza taharuki kwa jamiii kwani inaleta sintofahamu kwa baadhi ya wazazi.

Agizo hilo amelitoa Julai, 24, 2024 ambapo amesema hivi karibuni Temeke kulitokea tukio la mama kiziwi kupigwa na wananchi pasipokuwa na hatia akisingiziwa kuwa ni mtekaji watoto na alihojiwa na polisi na kugundulika kuwa ni kiziwi na alipohojiwa kumbe alikuwa anauliza tu .

"Kwa kweli mimi nimechukizwa sana na baadhi ya vyombo vya habari namna wanavyoripoti matukio haya kwa kuzua taharuki hivyo nitafuatilia na kufikisha kwa mamlaka inayohusika nao ili wawajibishwe kisheria kwani tukiacha waendelee  italeta sintofahamu kwa Jamii" amesema Chalamila

Aidha Wananchi watambue kuna vyombo vya ulinzi na usalama  wa raia taarifa nyingine wazipuuze  kwani kumeibuka baadhi ya wakina mama walezi wamekuwa wakiwaficha watoto na kupigia baba zao simu ili watumiwe hela za matumizi hivyo wameshabainika na wameonywa na Jeshi la polisi ili tabia hiyo isijirudie

No comments:

Post a Comment

Pages