August 03, 2024

Serikali yashauriwa kuweka mkazo kwenye Kilimo Ikolojia

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma

                            
SERIKALI imeshauriwa kuweka mkazo kwenye kilimo ikolojia hai kwa kuwa ndio nguzo ya kilimo katika kunajenga umoja katika uzalishaji, haki za walaji,  viumbe hai na utunzaji wa mazingira ya chakula kinachotoka.                          

Ushauri huo umetolewa na Mtaalam wa Mbegu kutoka Shirika la Mtandao wa Baionuai Tanzania (TABIO), Daud Manongi, wakati akizungumza na mwaandishi wa habari hii kwenye maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayofanyika mkoani Dodoma. 
           
Manongi alisema iwapo serikali itaweka mkazo kwenye kilimo ikolojia hai, ni wazi itakuwa imegusa viumbe hao wote ambao wanahusika na sekta hiyo.     

                  
Alisema iwapo serikali itahakikisha wakulima wanalima kwa njia kilimo ikolojia  uzalishaji utakuwa wa muda mrefu, huku ardhi ikiwa salama na endelevu kwa vizazi vijavyo.
                                  
"Sisi wadau wa kilimo ikolojia hai tunaomba serikali iweke mkazo kwenye kilimo ikolojia hai, kwa sababu ndio nguzo ya kilimo kwa kujajenga umoja kwenye uzalishaji, haki za walaji, viumbe hai na utunzaji wa mazingira ya chakula linalotoka," amesema.                             

Manongi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Wadau wa Kilimo Ikolojia Kitaifa, alisema wameshiriki maonesho hayo ili kuonesha mchango wa wadau wa kilimo hicho.     

Alisema kilimo ikolojia kina mchango chaya katika kukuza sekta hiyo ambayo inahusisha zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania.                        

Manongi alisema kwa siku za karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya tabianchi ambayo yameathiri mifumo ya kilimo, hivyo njia ya kurejea kwenye kilimo chenye tija ni kilimo ikolojia hai.               

Alisema wadau wa kilimo ikolojia hai wamebeba ujumbe wa mbegu ni uhai kwa lengo la kuhakikisha wadau wote wanashiriki kuzilinda, kuzitunza na kuziendeleza mbegu za asili, ikiwa ni kuendeleza urithi walioupokea.              

Mtaalam huyo alisema katika maonesho hayo wamehusisha mashariki 17 ambayo ni TABIO, Mtandao wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM) SJS Organic, McDonald, Inades, Floresta, IDP, KPC, Kijani Hai, Farm Redio International, Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania (SAT), Shirikisho la Wakulima Tanzania (SHIWAKUTA), PELUM, Agroecology Hub Tanzania, Biovision  Trust, Safari Organic Fertilezer na Via Agroforest.
                           
Manongi alisema mfumo wa kilimo ikolojia hai unasaidia uhakika wa masoko kwa mazao ndani na nje ya nchi.          

Mratibu wa TABIO, Abdallah Mkindi alisema wao kama wadau wa kilimo ikolojia wataonesha mazao mbalimbali ambayo yanatokana na kilimo hicho.      

                          
Mkindi alisema katika maonesho hayo wameleta zaidi ya aina 80 za mbegu za asili ambazo zikipewa mkazo na kuwekewa mkakati maalumu, zitaeda kuleta mapinduzi chanya kwenye mfumo wa chakula.                                

"Tungependa serekali iweke mkazo katika viuatilifu vya asili ili kudhibiti vifumbuzi vya mimea, hasa katika kipindi hiki ambacho kuna changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi," alisema. 

                               
Mratibu huyo alisema pia wanatumia maonesho hayo kuhakikisha elimu ya mbegu za asili inatolewa ili wakulima waweze kujua faida.              

Kwa upande wake Meneja Miradi Msaidizi wa SAT, Daudi Gwabara alisema wanatumia maonesho hayo kuithibitishia serikali na umma namna kilimo ikolojia hai kilivyo na faida iwapo kikipewa mkazo.                                 

"Sisi tunaomba wakulima na serikali waanze kubadilika kwani ushahidi umeonesha kilimo cha kisasa hakina tija, hivyo tuwekeze kwenye kilimo ikolojia hai ambacho kina faida kwa afya ya binadamu, ardhi na viumbe wengine," alisema.                                

Gwabara alisema ardhi yenye kemikali za viwandani inaenda kuumiza kizazi kijacho katika mavuno, hivyo ni wakati muafaka kujikita kwenye kilimo hai.    

          
Alisema SAT inahusisha wakulima 3,000 nchini kote ambao wanalima eneo lenye ukubwa wa heka 900.                             

Ofisa Uchechemuzi wa TOAM, Paul Chilewa alisema pamoja na mambo mengine wao kama wadau wa kilimo ikolojia wanaitaka serikali itekeleze Mkakati wa Kilimo Ikolojia Hai ambao ulizinduliwa mwaka jana, wenye vipambele vya upatikanaji wa pembejeo, masoko, utafiti wa teknolojia na kusambaza elimu ya ugani.     

"Kilio chetu sisi ni kuiomba serikali ianze utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia Hai ambao umeonesha njia ya sisi kupita katika kumkomboa mkulima na walaji, kwa kutenga rasilimali fedha na watu," alisema



No comments:

Post a Comment

Pages