Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amefunga Onesho la Nane
la Utalii la Kimataifa la Swahili kwa kuwahimiza Watanzania kuzitunza
na kuhifadhi rasilimali zilizopo nchini ili kuendelea kukuza Sekta ya
Utalii.
Balozi
Dkt Chana ametoa rai hiyo Jijini Dar es salaam wakati akifunga Onesho
la nane la Utalii la Kimataifa la Swahili ( S!TE) ambalo limefanyika
kuanzia Oktoba 11 ,2024 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini humo
Amesema
kuwa utalii na ulinzi wa rasilimali za Nchi yetu ni kipaumbele cha Kila
mtanzania,hivyo hakuna budi kuhakikisha kila mtanzania anafanya hivyo
ili kukuza sekta ya utalii.
"Tukizungumzia
suala la utalii kila mtu ananufaika,kwanza shirika la ndege ATCL
linapata abiria wengi wanaokuja kutalii nchini hapa,,pia mtalii
anaposhuka anatumia usafiri wa ndani ambapo madereva wananufaika,hivyo
hivyo ananunua bidhaa mbalimbali,hata mkulima mdogomdogo huko kijijini
ananufaika kwa uuza mazao yake,huu ni mnyororo mkubwa wa thamani katika
sekta ya Utalii." Amesema
Nakuongeza
kuwa Tanzania tuna vivutio vingi ,kuna Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu
kuliko yote Afrika Mashariki, tuna Utalii wa fukwe,mali kale, pia tuna
hifadhi za National Parks zisizopungua 21, makumbusho za Taifa
zisizopungua saba.
Amesisitiza
kuwa kadri siku zinavyokwenda watalii wanazidi kuongezeka ambapo kauli
mbiu ya onesho la S!TE mwaka huu " Utalii na Amani" ambapo Tanzania ni
kisiwa Cha amani na imekua mfano katika nchi za Afrika Mashariki na
SDAC.
Hata
hivyo Balozi Dkt. Chana ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watanzania kwa
kuendelea kudumisha amani na utilivu pamoja na kuendeleza kudumisha
mila na desturi za kitanzania kwani imekua chachu kubwa ya kuvutia
watalii.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Dkt. Ramadhan Dau amesema kuwa onesho la mwaka huu limepata mafanikio makubwa
ukilinganisha nala Mwaka Jana kutokana na wanunuzi wa vifaa vya Utalii
kuongezeka,makampuni ya kufanya maonesho,
"Kama
alivyosema waziri,kwenye utalii kuna mambo mawili ,kwanza
kuhifadhi,pili kutangaza utalii,na sisi TTB kazi yetu kubwa ni kutangaza
utalii nje ya nchi na hata kwa watanzania wenyewe,lakini pamoja na hili
la uhifadhi kua lipo kwenye Wizara yetu lakini ni jukumu la kila
mtanzania kuhifadhi rasilimali" amesema Balozi Dr.Dau
Nae,
Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Misitu (TFS), Profesa Dos Santos Silayo
amesema Utalii wao kwa kiasi kikubwa upo kwenye Mazingira Ikolojia
ambayo ni ya kuona na kuushughulisha mwili na akili hususani kwenye
masuala ya kutembea kwenye Misitu, kupumzika, kupanda milima na michezo
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment