November 20, 2024

Barrick yatunukiwa Tuzo ya mdhamini mkuu wa Mkutano wa Kimataifa wa Madini Tanzania 2024

Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akikabidhi cheti cha tuzo ya udhamini mkuu wa mkutano wa kimataifa wa sekta ya madini kwa Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo ya udhamini wa mkutano wa kimataifa wa sekta ya madini unaoendelea nchini.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa sekta ya madini nchini akipata maelezo ya shughuli za Barrick kwenye banda la maonesho la kampuni hiyo lililopo katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Dhahabu ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals, imetunikiwa tuzo ya udhamini mkuu wa mkutano wa uwekezaji katika sekta ya Madini Tanzania unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo kwa makampuni yaliyodhamini mkutano huu mkubwa wa kimataifa wa sekta ya madini zimekabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt.Samia Suluhu Hassan, baada ya ufunguzi wa mkutano huo

Mkutano huo mkubwa wa kimataifa unawakutanisha wadau wa madini wanaojishughulisha na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani madini, wasimamizi wa Sekta kutoka Serikalini, watoa huduma migodini na wafanyabiashara na kauli mbiu yake mwaka huu ni “Uongezaji wa Thamani ya Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi”.

Akiongea katika mkutano huo kabla ya kukabidhiwa tuzo hizo, Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, amewaeleza wajumbe wa mkutano huo jinsi ubia wa Barrick na Twiga unavyoendelea kupata mafanikio makubwa na kuwa mfano wa kimataifa unaodhihirisha kuwa Serikali inaweza kushirikiana na sekta binafsi na kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi.

Ngido, ameeleza kuwa katika kipindi kifupi kupitia ubia huu, umeweza kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa kupitia kodi na tozo mbalimbali za Serikali, kuongeza ajira kwa watanzania, kufanikisha miradi mikubwa ya kijamii hususani katika sekta ya barabara, afya, maji, na elimu pia umefanikisha kuinua uchumi wa wazabuni wa kitanzania wanaouza bidhaa mbalimbali kwenye migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi

No comments:

Post a Comment

Pages