MABAO mawili yaliyowekwa kambani na Prince Mpumelelo Dube na Pacome Pedow Zouzoua, yametosha kuwapa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara - Yanga ushindi wa 2-0 dhidi ya Fountain Gate FC ya Babati mkoani Manyara.
Penalti iliyopivwa kiufundi na Dube ilitokana na beki Derick Mukombozi wa Fountain Gate kuunawa mpira ndani ya boksi, huku Pacome yeye kwa upande wake akimalizia kimiani pasi elekezi ya Abuya, ambaye alinufaika na kazi ya ziada iliuofanywa na beki Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' aliyeingia akichukua nafasi ya Shedrack Boka.
Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 13 na kupanda hadi nafasi ya tatu ya msimamo, ikizishusha Namungo FC (yenye alama 12) na Mashujaa FC 'Wazee wa Mapigo na Mwendo' (wenye pointi 13), huku Fountain ambao waliingia dimbani wakiwa na alama sawa na Yanga, wakibaki na alama zao 10 nafasi ya saba.


No comments:
Post a Comment