NMB yatoa
500m/- kusaidia matibabu ya moyo ya watoto 125 nchini
Na
Mwandishi Maalum
Benki
ya NMB tayari imetoa nusu ya TZS bilioni 1 ilizoahidi mwaka jana kwa ajili ya kuiwezesha Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa matibabu
ya moyo ya watoto 250 katika kipindi cha miaka minne, hatua ambayo imesaidia kubadili
maisha ya familia zisizojiweza nchini.
Ahadi
hiyo, iliyotolewa tarehe 2 Novemba mwaka jana, inalenga kugharamia upasuaji na
matibabu ya watoto wanaokabiliwa na magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo na
matatizo mengine ya mfumo wa moyo, hususan wale wanaotoka katika familia
zenye kipato duni.
Jana,
Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa
NMB, Bi. Ruth Zaipuna, aliongoza ujumbe wa maafisa
waandamizi wa benki hiyo kutembelea JKCI, ambapo alitangaza kuwa benki hiyo imeshatoa TZS
milioni 500 ambayo ni sawa na nusu ya ahadi yote.
Kwa
mujibu wa Bi Zaipuna, kiasi hicho kimesaidia kuwezesha upasuaji na matibabu ya
moyo ya watoto 125.
“Tunawashukuru
sana JKCI kwa kazi yao ya kipekee ya kufanya upasuaji huuna tunaahidi
kuendeleza ushirikiano huu ili kuwasaidia Watanzania hasa familia
zisizojiweza kupata matibabu na huduma stahiki,” alsiema.
Aliongeza
kuwa kiasi kingine cha TZS milioni 250 kitatolewa Januari mwakani ili kuhakikisha
mchakato wa matibabu magonjwa ya moyo ya ya
watoto unaoendelea na kufanyika bila kukwama.
Bi Zaipuna
pia alisisitiza kuwa msaada wa NMB hauishii kwenye fedha pekee.
Benki
hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano
wake na JKCI, Heart Team Africa Foundation, na Global Medicare ili kupanua wigo
wa huduma, kuongeza kasi ya upasuaji, na kuimarisha miundombinu ya huduma za
moyo kwa watoto.
Moja
ya mapendekezo na maombi aliyoyapokea ni suala la kuanzisha “Recovery House” —
kituo maalum cha kuwapokea watoto wanaosubiri upasuaji au kuendelea
na matibabu — ambacho kitasaidia kupunguza mzigo wa kifedha na changamoto za
makaazi kwa familia kutoka maeneo ya
mbali.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, alisema NMB
imekuwa mdau namba moja katika kusaidia familia zisizojiweza kupata huduma
muhimu za moyo.
Bingwa
huyo wa magonjwa ya moyo alibainisha kuwa mchango wa benki hiyoumeongeza
ufanisi wa huduma, kupunguza muda wa kusubiri na kuongeza idadi ya watoto
wanaoweza kutibiwa kila mwaka.
Kwa
upande wake, Afisa Mgtendaji Mkuu wa
Heart Team Africa Foundation, Dkt. Naizihijwa Majani, alisema ufadhili wa NMB umewanufaisha
watoto kutoka mikoa 20.
“Kati
ya upasuaji 185 uliofanyika mwaka huu, 125 wamefadhiliwa na NMB — jambo
linalothibitisha ukubwa wa uhitaji na thamani ya msaada unaotolewa kwa wakati,”
alibainisha.
Kwa
akina mama Veronica Temba na Asimina Issa kutoka Kilimanjaro, msaada huo
umekuwa mwanga wa matumaini. Wakiwa hawana uwezo wa kugharamia upasuaji wa
moyo, waliuelezea mchango wa NMB kama “baraka ya kweli” kwa familia zao.
Wameiomba
benki hiyo kuendeleza moyo huo wa ukarimu ili familia nyingine nyingi zisizo na
uwezo ziendelee kunufaika na ufadhili wa matibabu ya moyo - ufadhili ambao kwa
wengi wao ndio tofauti kati ya kukata tamaa na kupata matumaini mapya ya
maisha.
Ziara
hiyo ilibainisha ukweli muhimu: mpango wa NMB wa kusaidia matibabu ya moyo ya
watoto sio tu jukumu la kijamii — ni uwekezaji katika kizazi kijacho cha
Tanzania, na katika maisha ya watoto ambao vinginevyo wangeachwa bila
matumaini.





No comments:
Post a Comment