HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 05, 2026

MBETO: CCM IMEJIJENGA TAASISI IMARA YA KISIASA

Mwandishi  Wetu, Zanzibar 


CHAMA Cha Mapinduzi  ( CCM) kimesema wakati ifikapo 05 Februari 2026 kikitimiza miaka 49 toka kuzaliwa kwake 1977, kinajivunia juhudi za  kufikia shabaha na malengo ya kuundwa kwake.


Chama hicho kinasisitiza kuendelea kusimamia  misingi ya Sera zake kwa kuendelea  kuhubiri tija na  faida ya ustawi wa amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.


Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis  Mbeto Khamis anaeza misingi ya chama hicho leo 04 Februari 2026,  akiwa Ofisi Kuu ya CCM  Kisiwandui.



Mbeto anasema kwa Miaka 49 Serikali  za CCM  zimemfanya  mTanzania atoke katika kadhia ya unyonge wa kunyonywa, kunyanyaswa na kudharauliwa hadi kuwa  mtu huru anayeheshimika. 


CCM katika kuamini Umoja wa Afrika (AU), anasema Mbeto, kimeshiriki kikamilifu katika harakati  zilizoleta Ukombozi wa Mataifa karibu yote yaliyopo, Kusini mwa Afrika.


Miaka 49 ya Sera za CCM, mTanzania amewekwa mbali   Mtanzania amewekwa mbali na maadui  Ujinga, Umasikini na Maradhi.


"Tunaelewa  maadui hao ni kazi kumalizika kwa pamoja, mapambano  dhidi yao  yataendelea" anasema Mbeto.


Anabainisha kuwa, umadhubuti wa CCM  utabaki katika  kuziunganisha jamii, kufuta   aina zote za   unyonyaji, maonevu au  jaribio lolote la  kudhoofisha uchumi na kuzorotesha maendeleo.


"Kuwepo kwa  vituo vya afya, zahanati na  hospitali  ni kumkabili adui  maradhi. Kujenga   Shule za Msingi na Vyuo Vikuu ni mkakati wa  kufuta Ujinga.


Anasema Mwenezi Mbeto, miradi ya kilimo, uvuvi, ufugaji, ujenzi wa viwanda, barabara na masoko ni kumfanya kila mtu ajijenge kiuchumi.


Kuhusiana na  ustawi wa maendeleo ya  demokrasia ndani ya CCM, anasema  ushiriki wa wanachama katika kuamua, kuchagua na kuchaguliwa ni kielelezo cha kukomaa kwa tasisisi hiyo.


'Kwa miaka 49 tumejenga  taasisi  imara, makini  inayoaminiwa na kutegemewa na  Wananchi wote. Pia sera na miongozo ya  chama chetu  imekuwa ikibadilka kulingana na mahitaji ya nyakati"  anasema Mwenezi Mbeto ambaye chama chake hicho ndio kimekuwa kikiisimamia serikali katika kutekeleza Ilani na Sera za CCM kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages