Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe pamoja
na Rais wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço kama ishara ya
uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital
dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda,
Angola, tarehe 01 Agosti, 2026. Kulia ni Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa
Taifa akishuhudia tukio hilo. Hospitali hiyo imepewa jina la Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama heshima na ishara ya kutambua
mchango wake katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, hususan nchi za Kusini
mwa Afrika, ikiwemo Angola.


No comments:
Post a Comment