Na Christopher Siwingwa
Waziri wa Nishati mheshimiwa Dkt Juma Homera, amesema serikali imetenga shilingi Trillion 2.46 sawa ma aslimia 97.5 ya bajeti ya wizara ya nishati kwa mwaka wa Fedha 2027/27 kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo ya nishati..jpeg)
Waziri Homera amesema hayo wakati wa ufunguzi wa maenesho ya 10 ya kimataifa ya biashara ya Nishati ya umeme ( Power and Solar Energy expo International Trade) yaliofanyika jijini Dar es salaam.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya serikali kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya uhakika na kutosha na kukidhi wananchi katika shughuli za kiuchumi.
Mheshimiwa Dkt Homera amesema serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka msukumo katika kukuza sekta ya nishati ili kichocheo na ukuaji wa uchimi na ustwawi wa wananchi.
Ameongeza kuwa kupitia bajeti hiyo serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo miradi ya kufua umeme wa maji katika bwawa la Mwalimu Nyerere pamoja na mradi wa umeme jua uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, ambapo megawati 50 tayari zimeunganishwa kwenye gridi ya Taifa na awamu ya pili inatarajiwa kuomgezwa megawati 100.
Aidha amesema serikali itaendelea kutekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia mwaka 2024-2034 yenye lengo la kuhakikisha aslimia 80 ya Watanzania wanatimia nishati safi ifikapo 2034.
Ametaja miradi ya umeme vijijini kupitia mpango wa kupeleka umeme katika vitongoji 9009 ifikapo mwaka 2030 kwa gharama ya shilingi Trillion 12 pamoja na kuimalisha mchanganyiko wa vyanzo vya nishati.
.jpeg)

No comments:
Post a Comment