January 26, 2013

AFCON 2013: BURKINA FASO YAISASAMBUA ETHIOPIA 4-0


Alain Traore wa mali aliyesimama akishangilia kwa staili ya kufutwa vumbi viatu pamoja na Florent Rouamba. Burkina Faso iliichapa Ethiopia mabao 4-0.

JOHANNESBURG, Afrika Kusini

Mapema hiyo jana, mabingwa watetezi waliponea chupuchupu, baada ya kusawazisha mwishoni na kuambualia sare ya 1-1 dhidi ya Nigeria, katika mechi ambayo kiungo John Obi Mikel alikosa penati, huku kipa Kenedy Mweene akisawazishia Zambia kwa njia hiyo

NYOTA Alain Traore alifunga mara mbili dakika za 33 na 73 na kuwawezesha wachezaji 10 wa kikosi cha Burkina Faso juzi usiku kushinda mabao 4-0 dhidi ya Ethiopia na kuhitimisha mfululizo wa mechi 18 bila ushindi katika Mataifa Afrika.

Ushindi wa mwisho wa Burkina Faso ulipatikana mwaka 1998, lakini juzi Traore, pamoja na Kone aliyefunga dakika ya 78 na Pitroipa dakika ya 90, walihitimisha jinamizi hilo na kuipaisha timu yao kileleni mwa msimamo wa kundi C kwa kufikisha pointi 4.

Mapema hiyo jana, mabingwa watetezi waliponea chupuchupu, baada ya kusawazisha mwishoni na kuambualia sare ya 1-1 dhidi ya Nigeria, katika mechi ambayo kiungo John Obi Mikel alikosa penati, huku kipa Kenedy Mweene akisawazishia Zambia kwa njia hiyo.
 
Kocha wa Burkina Faso, Mbelgiji Paul Put, alifurahishwa na matokeo ya mechi yao, yaliyowaweka juu ya kundi hilo linalojumuisha pia timu za Zambia, Nigeria na Ethiopia, ambapo sasa Burkina itamaliza na Zambia, huku Nigeria ikilaruana na Ethiopia hapo Jumanne Januari 29.

No comments:

Post a Comment

Pages