January 26, 2013

RAIS REAL MADRID: HAKUNA SHINIKIZO KWA JOSE MOURINHO


MADRID, Hispania

“Ni uongo kabisa kwamba mimi, nahodha na Mkurugenzi Mkuu tulikutana wakati wa chakula cha mchana, kwa ajili ya pamoja na mambo mengine kumjadili Mourinho kama kocha”

REAL Madrid juzi usiku imelazimika kukanusha habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuwa iliwauliza wachezaji wake nyota na waandamizi kama imfukuze kazi majira ya joto kocha wao Jose Mourinho.

Rais wa Madrid, Florentino Perez (pichani kushoto) ameyakana madai kwamba nahodha wa Galacticos, Iker Casillas na Sergio Ramos wamemwambia kwamba wachezaji nyota kikosini wataomba kutimka Bernabeu, kama klabu itaendelea kuwa chini ya Mourinho msimu ujao.

Perez alisema: “Ni uongo kabisa kwamba mimi, nahodha na Mkurugenzi Mkuu tulikutana wakati wa chakula cha mchana, kwa ajili ya pamoja na mambo mengine kumjadili Mourinho kama kocha.

“Uliochapishwa magazetini ni uongo wenye nia ya kutibua utulivu wa klabu yetu,” aliisistiza Perez.

Mourinho ameripotiwa kugombana na wachezaji nyota wa Madrid, wakiwamo Cristiano Ronaldo, Ramos, Pepe, Mesut Ozil, Fabio Coentrao na Casillas, ambaye atakosa mechi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man United baada ya kuumia mkono wa kushoto.

Kutokana na kuumia na kutarajiwa kukosekana kikosini kwa Casillas langoni, Mourinho amedaiwa kufikiria kutoa dau nono la pauni milioni 10 kuwania saini ya mlinda mlango wa Spurs, Mfaransa Hugo Lloris ama Mbrazil wa QPR, Julio Cesar.

….The Sun…..

No comments:

Post a Comment

Pages