January 04, 2013

AFCON 2013: IVORY COAST WASAKA NGUVU MISIKITINI/MAKANISANI


 Kikosi cha Ivory Coast kilichoshiriki fainali za Mataifa Afrika 2012 nchini Gabon/Equatorial Guinnea

 ABIDJAN, Ivory Coast

VIONGOZI wa Shirikisho la soka la nchini hapa, juzi walifanya ziara kwenye nyumba za ibada kuomba baraka kwa ajili ya timu ya taifa iweze kufanya vizuri kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

Hiyo imekuja zikisalia siku 17 kabla ya kuanza kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19.

Kwa kutambua umuhimu wa baraka za Mungu kwa jambo lolote lile, viongozi hao walifanya ziara kwenye makanisa namisikiti.

Kwa mujibu wa jopo hilo chini ya Rais wa Shirikisho la soka la hapa, Sidy Diallo, sara ni kitu muhimu katika fainali hizo ili timu hiyo iweze kupata mafanikio ya ubingwa.

Licha ya timu hiyo kutinga fainali katika michuano iliyopita nchini Gabon naGuinea ya Ikweta, ilifungwa na Zambia kwa mikwaju ya penalti.

“Tumekuja kwenu kuomba baraka za mwaka 2013 kuelekea fainali za Afrika, tukiamini maombi yenu yataiwezesha timu kupata mafanikio,” alisema Diallo mbele ya Mchungaji Ediemou Blin, rais wa Umoja wa vyombo vya kidini. 

Diallo alisema kwa upande wa uwezo na afya za wachezaji wa timu hiyo, hana hofu hivyo wamefika kwenye nyumba za ibada kuomba baraka za Mungu.

Ivory Coast itakayoshiriki fainali hizo kwa mara ya 20, kuanzia Januari 6 hadi 16, itakuwa Abu Dhabi kwa kambi na kuchyeza mechi za kirafiki ikiwemo dhidi ya Misri. 

Wakati hayo yakiendelea, Kocha Sabri Lamouchi ametaja kikosi cha mwisho cha nyota 23, wakiwemo wakongwe chini ya nahodha wake Didier Drogba.

Ivory Coast iliyopo kundi D pamoja na timu za Algeria, Togo  na Tunisia, itaanza kamperni yake Januari 22 dhidi ya Togo.

Nyota waliomo kwenye kikosi cha Ivory Coast, ni makipa: Barry Boubacar, Yeboah Daniel na Sangare Badra Ali. 

Mabeki: Bamba Souleman, Boka Arthur, Eboue Emmanuel, Lolo Igor, Tiene Siaka, Toure Kolo Abib na Ismael Traore 

Viungo: Abdul Razak, N’Dri Koffi Romaric, Max Gradel, Tiote Cheik Ismael, Toure Yaya Gnegneri, Ya Konan Didier na  Zokora Didier 

Washambuliaji: Drogba Didier, Salomon Kalou, Kone Arouna, Traore Lacina, Bony Wilfried na Yao Kouassi Gervais

No comments:

Post a Comment

Pages