January 11, 2013

Beatrice Mathew ‘Nabisha’ anajipanga kuachia wimbo wake mpya



Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Beatrice Mathew ‘Nabisha’ anajipanga kuachia wimbo wake mpya ambao hajataka kuutaja jina lake kutokana na kuwepo na wizi wa mawazo ya wenzao katika tasnia hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nabisha alisema kwasasa yupo kwenye michakato ya kutengeneza video ya wimbo huo.

“Sipendi kutaja jina la wimbo wangu maana kuna watu wamekaa tayari kwa ajili kuangalia nani anafanya nini kwa wakati gani” alisema Nabisha.

Aliwaomba wasanii kuwa na moyo wa kujituma katika kazi zao na kuwa na fikra za mbali ambazo zitawawezesha kufanya kazi zenye ujumbe katika jamii.

Mbali na maandalizi hayo, Nabisha alishawahi tamba na nyimbo zake kama Kidole gumba na nyinginezo ambazo zilimtambulisha vyema katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment

Pages