January 11, 2013

SUMA LEE KUTOKA NA 'UTAMU'


Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na wimbo wake wa ‘Asiyecheza atoke’ nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail Seif  ‘Suma Lee’ ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Utamu’ mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Suma Lee alisema wimbo huo kamshirikisha Khalifani Majani ‘P.Funk’ ambae amemsapoti vilivyo na anaamini utafanya vizuri kutokana na ujumbe uliopo ndani ya wimbo huo.

Suma Lee aliwataka mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kuusikiliza na kuuangalia wimbo huo kwani unajumbe na unaburudisha kwa yeyote atakaye uona.

“Nawaomba mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti kwani kuna vitu vizuri nilivyowaandalia ambavyo vitakua tofauti kabisa na haviwezi kuelekeana na hakunaga” alisema Suma Lee.

Mbali na wimbo huo, Suma Lee alishawahi tamba na nyimbo zake kama Hakunaga, Chungwa na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment

Pages