January 02, 2013

Benard Paul ‘Ben Pol kutoka na Linnah


Na Elizabeth John
Mkali wa RnB nchini, Benard Paul ‘Ben Pol’ anajipanga kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Yatakwisha’ ambacho kamshirikisha msanii wa muziki huo, Estelina Sanga ‘Linnah’.

Akizungumza Dar es Salaam, Ben Pol alisema  yupo katika maandalizi ya kufanya video ya kazi hiyo ambapo ataachia audio pamoja na video ya kazi hiyo, mwishoni mwa mwezi huu.

“Sijawahi kumshirikisha msanii yeyote katika kazi zangu, hii ndio kazi ya kwanza, nimeamua kumshirikisha kwa lengo la kutoa burudani iliyotofauti kwa mashabiki wangu, hivyo naomba wakae mkao wa kula kwaajili yakuipokea kazi hiyo,” alisema Ben Pol.

Alisema kazi hiyo amerekodia hapa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Morogoro, na anaomba wapenzi wa RnB nchini waendelee kumpa sapoti katika kazi zake ambazo zinakuja.

Mbali na kazi hiyo, Ben Pol alishawahi kutamba na kazi zake nyingi ukiwemo ya ‘Pete’ ambayo inafanya vizuri kwasasa huku Linnah akitamba na kazi yake inayokwenda kwa jana la ‘Ushanifahamu’.

No comments:

Post a Comment

Pages