January 02, 2013

KIUNO KUBEBA ALBAMU YA TID MNYAMA


Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Mohammed ‘TID Mnyama’ anajipanga kuachia albamu yake ya tatu inayokwenda kwa jina la ‘Kiuno’.

TID alishawahi kutamba na albamu zake mbili ikiwemo ya ‘Nyota yangu’ ambayo ilifanya vizuri na kumtangaza katika nchi za jirani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, TID alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na nyimbo zote zilizokuwepo humo kufanya vizuri katika soko hilo.

Alisema anawaomba mashabiki wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili kuipokea kazi hiyo ambayo imetengenezwa kwa kufuata maadili ya Mtanzania.

“Nafurahi kwasababu kazi zangu zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu naomba mashabiki wangu msichoke kunisiliza kwani bado kuna vitu vizuri ambavyo nawaanndalia,” alisema TID.

Mbali na kibao chake cha Kiuno ambacho kinabeba jiana la albamu hiyo, TID alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Nyota yangu’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri zaidi licha ya kuwa na vibao vingi.

No comments:

Post a Comment

Pages