January 07, 2013

BENITEZ KUWAPANGA PAMOJA TORRES NA DEMBA BA


 Demba Ba
Fernando Torres

LONDON, England

"Wanaweza kucheza pamoja safu ya mbele ya Chelsea. Ba alikuwa akicheza akiwa na Papiss Cisse katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa kucheza ushambuliaji pacha"

KOCHA Rafael Benitez amesema haoni sababu kwa nini washambuliaji wake Demba Ba na Fernando Torres wasiwezer kucheza pamoja kwa mafanikio, kauli aliyopitoa baada ya Ba kufunga mara mbili katiika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge Chelsea.

Ba, juzi lifunga mara mbili katika pambano la raundi ya tatu ya Kombe la FA, kuiwezesha Chelsea kuiondosha mashindanoni Southampton, kwa mabao 5-1 mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa St Mary’s.

Huku Torres akianzia benchi katika mechi hiyo ya Jumamosi, Ba ilimchukua takribani dakika 35 kufunga bao lake la kwanza kabisa akiwa na Chelsea, ambalo lilikuwa la kusawazisha na kufungua mvua ya mabao baadaye.

"Wanaweza kucheza pamoja safu ya mbele ya Chelsea," alisema Benitez baada ya mechi hiyo.

"Ba alikuwa akicheza akiwa na Papiss Cisse katika kikosi cha Newcastle, hivyo yeye anaweza kabisa kucheza ushambuliaji pacha na mwenzake kwa sababu ni mchezaji mjanja, lakinipia inategea na mfumo wa mchezo na nyota anaoshirikiana nao.

"Napendelea tatizo hili la kuwa na washambuliaji wawili, kuliko kupaswa kuwa na mmoja anayetakiwa kuwa makini mchezoni kwa dakika zote.

"Jambo muhimu kwa timu ni kuwa na wigo mpana wa uteuzi wa kikosi. Wao ni wachezaji wazuru na kimsingi wanaweza kupambana, au labda tunaweza kuwaongoza wao pamoja – inategemea na mchezo."

Ba alifunga bao moja katika kila kipindi, katika mechi ambayo kulikuwa na mabao kutoka kwa Victor Moses, Branislav Ivanovic na penati ya dakika za lala salama ya Frank Lampard.

"Ni muhimu mno kwa mshmabuliaji kufunga mabao, mengi zaidi awezavyo, lakini zaidi ni kwana nmna gani ushirikiano wake na timu unakuwa na uelewa alionao katika kuweza kutambua nini tunatarajia ambavyo vyote vimeniridhisha," alisema Benitez.

"Alionesha uzuri wake mbele ya lango na kila alichofanya dimbani katika mechi hii kilinivutia na kuniridhisha vya kutosha. Alikuwa mjanja mno mchezoni."

Aidha, bao la mtokea benchi Lampard katika mechi hiyo, lilimfanya aifikie rekodi ya utikisaji nyavu mara nyingi zaidi katika klabu hiyo kwa kufikisha mabao 193 na kumpiku mshikilia rekodi hiyo wa kudumu Kerry Dixon anayeshika nafasi ya pili sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages