January 07, 2013

MURRAY ATETEA UBINGWA WA BRISBANE INTERNATIONAL


Andy Murra akinyanyua juu taji lake la ubingwa wa Brisbane International 2013

BRISBANE, Australia

Murray alitinga kirahisi fainali ya michuano hiyo baada ya mpinzani wake katika mechi ya nusu fainali, Kei Nishikori kujitoa mchezoni kutokana na kuumia goti

NYOTA wa tenisi raia wa Uingereza, Andy Murray jana Jumapili amefanikiwa kuutetea ubingwa wake wa Brisbane International kwa ushindi wa seti mfululizo, dhidi ya mpinzani wake Grigor Dimitrov.

Murray, bingwa wa Michuano ya Wazi ya Marekani ‘US Open’ na kinara wa mchezo kwa viwango vya ubora, aliibuka mbabe kwa 7-6 (7-0) 6-4 katika mechi iliyopigwa kwa saa moja na nusu, dhidi ya Dimitrov raia wa Ubelgiji anayeshika nafasi ya 48 ya ubora.

Haikuwa rahisi kwa Mskochi Murray kuibuka na ubingwa huo, akifanya kazi ya ziada kutoka nyuma kumuwezsha kuongoza hadi nusu ya kwanza na kuja kushinda.

Murray alitinga kirahisi fainali ya michuano hiyo baada ya mpinzani wake katika mechi ya nusu fainali, Kei Nishikori kujitoa mchezoni kutokana na kuumia goti.

Murray aleyecheza fainali akiwa anashikilia nafasi ya tatu kidunia kwa ubora wa tenisi na namba moja kwa Uingereza, alirudi vema kutoka mapumziko na kutoka nyuma na kushinda 6-4 katika mechi za seti tano mfululizo.

Murray alikuwa katika michuano ya Brisbane International, kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mashindano ya Wazi ya Australia ‘Australian Open’, yatakayofanyika kwa wiki mbili kuanzia Januri 14 hadi 27, jijini Melbourne.

No comments:

Post a Comment

Pages