January 11, 2013

BINGWA WA MKANDA WA IBF KUJULIKANA LEO


Na Elizabeth John

IKIWA leo ni siku ya kumaliza ubishi kati ya bondia Mkenya, Mark Oliech na Mtanzania Thomasi Mashali, wapenzi wa ngumi wameshauriwa kufika kwa wingi kuangalia pambano hilo la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati ambalo litafanyika katika ukumbi wa Friends Corner uliopo Manzese jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kupima uzito jijini Dar es Salaam, Oliech alisema yeye amejipanga kama inavyohitajika, kwa mazoezi aliyofanya anauhakika atamnnyamazisha mpinzania wake katika raundi za mwanzo.

“Mimi sihitaji kujua historia ya Mashali, na hata aliyoyafanya nyuma naomba tusubili hiyo kesho (leo) wenyewe mtakua na majibu nina uhakika na mazoezi niliyofanya hivyo siwezi kuongea sana,” alisema Oliech.

Kwa upande wake, Mashali alisema yeye bado ananafasi kubwa ya kuutetea mkanda huo kwani anauhakika mpinzani wake hawezi kuupata kwa vyovyote, amewataka wapenzi wa ngumi kujitokeza kwa wingi kuangalia jinsi anavyomgaragaza Mkenya huyo.

“Unajua maneno mengi humaliza nguvu, mimi ni bingwa wa mkanda huo, siwezi kuuruhusu uende nchi nyingine nauhakika ntafanya vitu vya ajabu katika raundi za mwanzo,” alisema Mashali.

Pambano hilo limeandaliwa na Picktime media and intertainment company limited kwa kushirikiana na TPBO  

No comments:

Post a Comment

Pages