January 01, 2013

BOB JUNIOR KUJA NA KICHUNA


Na Elizabeth John

MTAYARISHAJI na Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Rahim Rummy ‘Bob Junior’ ameachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kichuna’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bob Junior alisema yeye kama msanii anahaki ya kuwapa burudani mashabiki wake hivyo anaendeleza burudani hizo.

“Kazi hii nimeshaisambaza katika vituo mbalimbali vya redio, kwasasa natayarisha video, ambayo ninaamini itakua poa zaidi naomba mashabiki waendelee kunipa sapoti katika kazi hii,” alisema Bob Junior.

Alisema anaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kupokea vitu vizuri kutoka kwake kwani kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia ikiwa ni pamoja na video ya wimbo huo.

Licha ya kutamba na kazi hiyo katika vituo mbalimbali vya redio, Bob Junior alishawahi kutamba na vibao vyake vingi kikiwemo cha Nichuum ambacho kinafanya vizuri katika muziki wa bongo fleva.

No comments:

Post a Comment

Pages