January 10, 2013

CHEGE KUACHIA VIDEO MPYA YA 'USWAZI TAKE AWAY'


Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka kundi la Wanaume Family ,Juma Said ‘Chege’ amesema kuwa yuko mbioni kuachia video ya wimbo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Uswazi Take Away’.

Akizungumza jijini  Dar es Salaam, Chege alisema kuwa audio ya wimbo tayari imekamilika na wiki hii ataanza mchakato wa kutengeneza video ya wimbo huo na pindi itakapo kamilika ataisambaza kwenye vituo vya redio.

“Nitaanza kuachia video kabla ya audio kutokana na kuamini kuwa ndio utaratibu mzuri wa kutangaza kazi, hali inayosaidi kufanya vizuri katika tasnia ya muziki, kwani ukifanya vema kwenye video, audio inakuwa rahisi kukubalika,” alisema Chege.

Msanii huyo licha ya kufanya vizuri na vibao mbalimbali kwa sasa anatamba na kibao kinachoitwa Mwanayumba ambacho kinaendelea kukonga nyongo za mashabiki kutokana na maudhui yake.

Chege anawaomba mashabiki kukaa mkao wa kula kusubili kazi hiyo ambayo ipo katika mchakato wa mwisho kukamilika kwa upande wa video wakati audio iko tayari na itaachiwa baada ya video kuanza kuonekana.

No comments:

Post a Comment

Pages